Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 17:47

Rais wa Zamani wa Tunisia ahukumiwa miaka 4 gerezani


Polisi wa Tunisia wakikabiliana na waandamanaji dhidi ya rais Kais Saied, mjini Tunis
Polisi wa Tunisia wakikabiliana na waandamanaji dhidi ya rais Kais Saied, mjini Tunis

Rais wa zamani wa Tunisia Moncef Marzouki amehukumiwa kifungo cha miaka 4 kwa kile kilchoelezewa kama kuvuruga usalama wa taifa hilo.

Marzouki, mwenye umri wa miaka 76, anayeishi uhamishoni nchini Ufaransa hakuwepo mahakamani wakati wa hukumu hiyo.

Wiki chache zilizopita, Marzouki aliukosoa utawala wa rais Kais Saied na kuitisha maandamano dhidi ya serikali.

Vyombo vya habari vya Tunisia vimeripoti kwamba Marzouki amekuwa na hatia kwa makosa ya kudumaza usalama wa taifa akiwa nje ya nchi na kuvuruga uhusiano wa kidiplomasia wa nchi hiyo.

Marzouki pia alisema kwamba lilikuwa jukumu lake kupambana dhidi ya utawala wa kidikteta nchini mwake hadi mwisho wa maisha yake. Hajasema kama amemueleza wakili kukata rufaa dhidi ya maamuzi hayo.

Wakili wa Marzouki, Lamia Khemiri, amesema kwamba rais huyo wa zamani hakutakiwa kufika mahakamani na hajui sababu za mahakama kumhukumu.

XS
SM
MD
LG