Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 23:20

Mahakama Tunisia yamhukumu Rais wa zamani kifungo cha miaka 4


Wananchi wanaompinga Rais wa Tunisia Kais Saied wakishiriki katika maandamano katika kile wanachosema alipindua serikali Julai 25, mjini Tunis, Tunisia Septemba 18, 2021.REUTERS/Zoubeir Souissi

Rais wa zamani wa Tunisia Moncef Marzouki amehukumiwa kifungo cha miaka 4 kwa kile kilchoelezewa kama kuvuruga usalama wa taifa hilo.

Marzouki, mwenye umri wa miaka 76, anayeishi uhamishoni nchini Ufaransa hakuwepo mahakamani wakati wa hukumu hiyo.

Wiki chache zilizopita, Marzouki aliukosoa utawala wa rais Kais Saied na kuitisha maandamano dhidi ya serikali.

Vyombo vya habari vya Tunisia vimeripoti kwamba Marzouki amekuwa na hatia kwa makosa ya kudumaza usalama wa taifa akiwa nje ya nchi na kuvuruga uhusiano wa kidiplomasia wa nchi hiyo.

Marzouki pia alisema kwamba lilikuwa jukumu lake kupambana dhidi ya utawala wa kidikteta nchini mwake hadi mwisho wa maisha yake. Hajasema kama amemueleza wakili kukata rufaa dhidi ya maamuzi hayo.

Wakili wa Marzouki, Lamia Khemiri, amesema kwamba rais huyo wa zamani hakutakiwa kufika mahakamani na hajui sababu za mahakama kumhukumu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG