Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 26, 2024 Local time: 10:54

Rais wa Tunisia atuewa serikali mpya


Rais Kais Saied wa Tunisia alipoktana ofisini mwake waziri mkuu mpya Najila Bouden Romdhane.
Rais Kais Saied wa Tunisia alipoktana ofisini mwake waziri mkuu mpya Najila Bouden Romdhane.

Rais wa Tunisia Kais Saied Jumatatu aliteua serikali mpya kwa amri ya kiutendaji, wiki 11 baada ya kumtimua serikali iliyokuwepo madarakani kupitia uchaguzi.

Rais wa Tunisia Kais Saied leo, Jumatatu aliteua serikali mpya kwa amri ya kiutendaji, wiki 11 baada ya kumtimua serikali iliyokuwepo madarakani kupitia uchaguzi.

Saied alimfuta kazi waziri mkuu, alisimamisha bunge na akajipa mamlaka ya kimahakama katika kile kinachotajwa na upinzani kua ni mapinduzi ya Julai 25.

Serikali hiyo mpya inaongozwa na Najla Bouden, waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa nchi hiyo ya Afrika Kaskazini, ambapo Saied amerudisha kwa kiasi kikubwa madaraka yake hata hivyo rais anadendelea kua mkuu wa utawala yeye mwenyewe.

Serikali mpya ilitangazwa siku moja baada ya karibu watu elfu 6 kuandamana kati kati ya mji mkuu wa Tunis kupinga kunyakua kwake madaraka.

XS
SM
MD
LG