Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 03:30

Jaji Tunisia amshutumu Rais Saied kwa kudumaza uhuru wa mahakama


Rais wa Tunisia, Kais Saied. Tunisia, Sept. 20, 2021.
Rais wa Tunisia, Kais Saied. Tunisia, Sept. 20, 2021.

Rais Saied alitangaza uamuzi huo usiku wa kuamkia Jumapili ikiwa ni hatua ya karibuni kuimarisha  mamlaka yake baada ya kulifuta bunge na kumfukuza kazi waziri mkuu  mwezi Julai na kuahidi kuirekebisha katiba ya kidemokrasia katika hatua ambazo wakosoaji wake wameita ni mapinduzi

Jaji wa cheo cha juu wa Tunisia alimshutumu Rais Kais Saied kwa kudumaza uhuru wa mahakama kinyume cha sheria kwa kuvunja baraza kuu la kisheria siku ya Jumapili na kuonya kwamba majaji hawatakaa kimya.

Rais Saied alitangaza uamuzi huo usiku wa kuamkia Jumapili ikiwa ni hatua ya karibuni kuimarisha mamlaka yake baada ya kulifuta bunge na kumfukuza kazi waziri mkuu mwezi Julai na kuahidi kuirekebisha katiba ya kidemokrasia katika hatua ambazo wakosoaji wake wameita ni mapinduzi.

Baraza kuu la mahakama lilikuwa chombo nadra cha serikali ambacho bado kingeweza kuwa na ushawishi huru kwa Saied, ambaye kwa miezi kadhaa aliikosoa mahakama kwa kuchelewesha maamuzi ya kesi za ufisadi na ugaidi.

Akizungumza na shirika la habari la Reuters katika majibu ya kwanza ya umma ya wajumbe wa baraza kuu la mahakama baada ya tamko la Rais Saied, mkuu wake Youssef Bouzakher alisema inawakilisha jaribio la kuwaweka majaji chini ya maelekezo ya rais.

XS
SM
MD
LG