Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 00:30

Mahakama ya ICC yaamrisha kukamatwa kwa kiongozi wa waasi Nourredine Adam


FILE - Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu huko The Hague, Uholanzi, Nov. 7, 2019.
FILE - Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu huko The Hague, Uholanzi, Nov. 7, 2019.

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa waasi wa Afrika ya Kati, Nourredine Adam, kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu uliofanywa wakati wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo mwaka 2013.

Anasakwa kwa uhalifu anaodaiwa kutekeleza alipokuwa waziri wa usalama wa nchi.

Uhalifu huo ni pamoja na mateso, kufungwa gerezani, kutoweka kwa watu na kutendewa kikatili katika vituo vya vizuizi vinavyoendeshwa na serikali iliyokuwa ikitawala wakati huo.

Adam ndiye kiongozi asiye rasmi wa chama cha Popular Front for the Renaissance of the Central African Republic (FPRC) kundi la waasi ambalo lilijiondoa katika muungano wa Waislamu wengi wa Seleka mwaka 2014.

Hati hiyo hapo awali ilitolewa na kutiwa muhuri Januari 2019 lakini majaji wa ICC sasa walikuwa wameamuru isitishwe, mahakama ilisema.

Wababe wawili wa zamani wa kivita wa Afrika ya Kati, Patrice-Edouard Ngaissona na Alfred Yekatom, ambaye aliongoza wanamgambo wa Anti-Balaka, kwa sasa wanakabiliwa kesi katika mahakama ya ICC kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

XS
SM
MD
LG