Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 06:15

Fatou Bensouda anamaliza muda wake katika mahakama ya ICC


Fatou Bensouda, mwendesha mashtaka mkuu wa ICC anayemaliza muda wake
Fatou Bensouda, mwendesha mashtaka mkuu wa ICC anayemaliza muda wake

Wakili Muingereza, Karim Khan ambaye alimtetea William Ruto katika kesi ya ghasia baada ya uchaguzi mkuu Kenya mwaka 2007 hadi 2008 ndie anayechukua nafasi na kuwa mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) yenye makao yake The Hague

Mwanamke wa kwanza na mwafrika wa kwanza ambaye ni mwendesha mashtaka mkuu wa pili wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) raia kutoka Gambia, Fatou Bensouda, anaondoka madarakani Jumanne. Yeye na mtangulizi wake walipongezwa kwa kusukuma mipaka ya mahakama ya The Hague kama mahakama ya uamuzi wa mwisho na alikumbana na upinzani mkubwa chini ya uangalizi wake.

Katika uongozi wake wa miaka tisa, Bensouda alisimamia kesi ambazo zilikuwa na matokea chanya ikiwemo kesi ya kwanza kufafanua shambulizi la urithi wa kitamaduni kama uhalifu wa vita. Lakini pia alishindwa katika kesi ya hali ya juu, dhidi ya Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo na Makamu Rais wa zamani wa Congo, Jean-Pierre Bemba.

Karim Khan, mwendesha mashtaka mkuu mtarajiwa wa ICC
Karim Khan, mwendesha mashtaka mkuu mtarajiwa wa ICC

Mwanzoni mwa kazi yake Bensouda alishuhudia mashtaka yakifutwa dhidi ya Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, na Makamu Rais wake William Ruto juu ya ghasia za baada ya uchaguzi mkuu Kenya mwaka 2007 hadi 2008 kwa sababu zilijumuisha shutuma za muingiliano wa kisiasa.

Wakili Muingereza, Karim Khan, ambaye alimtetea Ruto katika kesi hiyo ndie anachukua nafasi ya kuwa mwendesha mashtaka mkuu wa ICC.

XS
SM
MD
LG