Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 17:16

Kesi ya mauaji ya maelfu ya watu Dafur, Sudan yaanza kusikilizwa ICC


Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Karim Khan Picha: AFP)
Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Karim Khan Picha: AFP)

Kikao cha kwanza kusikiliza kesi ya uhalifu wa kivita katika jimbo la Dafur, kimeanza leo Jumatatu katika mahakama ya uhalifu wa kivita ya kimataifa ICC. Kikao hicho kinafanyika baada ya karibu miaka 20 kupita tangu jimbo la Dafur kukumbwa na machafuko yaliyopelekea vifo vya maelfu ya watu.

Kikao hicho kinafanyika baada ya karibu miaka 20 kupita tangu jimbo la Dafur kukumbwa na machafuko yaliyopelekea vifo vya maelfu ya watu.

Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman, aliyekuwa kamanda wa kundi la wapiganaji la Janjaweed anakabiliwa na mashtaka 31 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwemo mauaji, unajisi na mateso.

Waendesha mashtaka wanamshutumu Abd-Al-Rahman, kwa kuwa kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la Janjaweed, lililokuwa linaungwa mkono na serikali, wakati wa vita vya Dafur kati yam waka 2003 na 2004.

Abd-Al-Rahman amekanusha madai hayo.

Wakati wa kikao cha awali, wakili wake walisema kwamba Abd-Al-Rahman ameshitakiwa kimakosa na kwamba hakuwa na elimu ya kutosha kuelewa kwamba amri zilizokuwa zikitolewa zingeweza kusababisha uhalifu wa kivita.

Vita vya Darfur vilianza baada ya waasi ambao wengi wao walikuwa wa kabila za kiafrika, kuanza vita dhidi ya serikali, ambayo nayo ilijibu kwa mapigano yaliyoongozwa na kundi la Janjaweed ambalo lilikuwa la wapiganaji wa kiarabu. Zaidi ya watu 300,000 waliuawa na milioni 2 kuachwa bila makao.

XS
SM
MD
LG