Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 03:00

Mafuriko yazikumba baadhi ya sehemu za Umoja wa Falme za Kiarabu


Port of Fujairah
Port of Fujairah

Mafuriko yamepiga maeneo ya umoja wa falme za  kiarabu wakati nchi ikikumbwa na mvua kubwa.

Baadhi ya watu waliokwama ambao walishindwa kutoka katika nyumba zao kwenye miji ya Sharjah na Fujairah waliokolewa na askari wa ulinzi wa raia.

Mafuriko yaikumba baadhi ya miji ya UAE
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:28 0:00

Fujairah imeathiriwa vibaya kutokana na hali yake ya asili ya milima na miinuko.

Sharjah pia imeathiriwa wakati Dubai na Abu Dhabi zilishuhudia mvua kidogo.

Maafisa walitoa tahadhari ya mvua kwa wakazi kubaki nyumbani na kutofika maeneo ambayo yameelezwa kuwa na mafuriko kama vile mabonde.

Pia wametangaza makazi ya muda yatatolewa katika hoteli kwa wale watakaotakiwa kuondoka katika nyumba zao.

Hali ya hewa mbaya imeshuhudiwa nchini humo Jumatano ilitarajiwa kuendelea hivyo hadi leo alhamisi.

XS
SM
MD
LG