Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 10:58

Kamala Harris na Blinken wamewasilisha rambirambi kwa familia ya marehemu Rais wa UAE


Makamu Rais wa Marekani Kamala Harris akisalimiana na kumpa pole Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan, Mei 16, 2022.
Makamu Rais wa Marekani Kamala Harris akisalimiana na kumpa pole Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan, Mei 16, 2022.

Makamu wa Rais wa Marekani kamala Harris na waziri wa mambo ya nje Marekani Antony Blinken siku ya Jumatatu waliwasilisha rambirambi kwa familia ya marehemu Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan aliyefariki Ijumaa.

Harris na Blinken walikutana na Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan kaka wa kambo wa marehemu rais ambaye ni Rais mpya wa UAE ambaye tayari ni mtu mwenye ushawishi mkubwa katika mashariki ya kati na kwingineko.

Makamu wa Rais alielezea heshima na kumbukumbu ya Sheikh Khalifa ambaye alikuwa rafiki mzuri wa Marekani na mshirika anayeaminika katika tawala nyingi ofisi ya Harris ilisema katika taarifa yake. Pia Makamu wa Rais alimpongeza Sheikh Mohammed kwa kuchaguliwa kwake kama Rais wa UAE.

Baada ya mkutano huo Blinken alipata chakula cha jioni na waziri wa mambo ya nje Sheikh Abdullah Bin Zayed Al Nahyan.

XS
SM
MD
LG