Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:14

Makamu wa Rais Harris azuru UAE kuimarisha ushirikiano, atoa rambirambi


Makamu wa Rais Kamala Harris
Makamu wa Rais Kamala Harris

Wakati huo huo marais na mawaziri wakuu wanaendelea kuwasili UAE kutoka sehemu mbalimbali duniani kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi aliyetawala taifa hilo.

Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan mtawala wa muda mrefu alifariki Ijumaa akiwa na umri wa miaka 73 baada ya kuongoza mageuzi ya miaka mingi ya haraka ya nchi kuwa kitovu cha biashara duniani na kituo chenye nguvu katika ukanda huo.

Ujumbe huo wa Marekani pia umekwenda huko kama sehemu ya kupunguza mivutano na kuonyesha uungwaji mkono wakati uhusiano ambao umekuwa si mzuri sana chini ya Rais Joe Biden.

Makamu wa rais Harris amewaambia waandishi wa habari kabla ya kuondoka uwanja wa Andrews Air Force Base kwamba Marekani, inachukulia kwa umakini mkubwa kuimarishwa uhusiano na washarika wake wa UAE.
Makamu wa rais wa marekani alieleza haya: “Naongoza ujumbe huu kwa niaba ya Rais Joe Biden na utawala wetu kwa ajili ya kutoa heshima zetu za mwisho. Marekani inachukua kwa umakini mkubwa kuimarisha uhusiano wetu, na ushirikiano na UAE na tunakwenda huko kutoa heshima zetu za mwisho, lakini pia kama kuonyesha nia yetu ya dhati na kuimarisha uhusiano huo na kuendelea kuuimarisha.’

XS
SM
MD
LG