Kiongozi huyo alifariki akiwa na umri wa miaka 73 baada ya kuugua kwa miaka mingi.
Kwa mujibu wa katiba ya nchi makamu rais na kiongozi wa Dubai Sheikh Mohammed bin Rashid al-Maktoum atakuwa kaimu rais hadi pale baraza la taifa la wafalme 7 watakapokutana katika muda wa siku 30 ili kumchagua rais mpya.
Nafasi ya kiongozi huyo wa taifa hilo lenye utajiri wa mafuta ambaye hakuonekana hadharani kwa muda mrefu huenda ikachukuliwa na kaka yake wa kambo mwana mfalme Mohammaed bin Zayed al Nahyan, ambaye tayari anachukuliwa kama kiongozi wa Emarati.
Wizara ya masuala ya Rais imetangaza siku 40 za maombolezo na bendera kupeperushwa nusu mlingoti na kazi za umma na sekta za binafsi zitafungwa kwa siku tatu.
Salamu za Rambi rambi zimeanza kuwasili na rais Joe Biden wa Marekani amepeleka salamu zake akimtaja Mfalme Zayed Al-Nahyan alikuwa mshirika wa kweli na rafiki wa Marekani.