Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 10:01

Filamu ya Walt Disney yapigwa marufuku UAE


Nembo ya Walt Disney
Nembo ya Walt Disney

Umoja wa falme za kiarabu Jumatatu umepiga marufuku filamu mpya ya Walt Disney ya Lightyear, iliyokuwa imepangwa kuzinduliwa wiki hii, tasisi ya serikali imesema.

Wizara ya vijana na utamaduni kupitia ujumbe wa twitter imesema kwamba filamu hiyo imekiuka maadili ya kijamii, bila kutoa maelezo zaidi. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters filamu hiyo ilikuwa imepangwa kuzinduliwa Juni 16 wakati matangazo ya uzinduzi wake yakiwa tayari yametolewa.

Filamu yenyewe inasemakana kuonyesha wanawake wawili wakibusiana ambao wana mahusiano ya kimapenzi. Sawa na mataifa mengine ya kiarabu, mapenzi ya jinsia moja hayakubaliki kwenye Umoja wa falme za kiarabu.

Serikali ya UAE pamoja na kampuni ya Disney inayomiliki filamu hiyo hawajatoa tamko lolote baada ya hatua hiyo. Hashtag ya kupigwa marufuku kwa movie ya Lightyear imekuwa ikitanda sana kwenye twitter baada ya tangazo hilo.

XS
SM
MD
LG