Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 20:54

Maandamano nchi nzima kupinga utawala wa Iran yaendelea kwa siku 33 mfululizo


Wanawake wakikimbia askari wa kuzuia ghasia wakati wa maandamano ya kupiga serikali mjini Tehran. Picha hii imepigwa na mtu ambaye siyo mfanyakazi wa shirika la habari la AP, Septemba 19, 2022.

Maandamano nchini kote Iran yanaendelea kwa siku ya 33 mfululizo, kufuatia kifo cha msichana aliyefariki akiwa chini ya ulinzi wa  polisi, huku watu wakiandamana usiku kucha katika  miji ya Tehran, Sanandaj na Dehgolan.

Waandamanaji hao walikuwa wakipiga kelele kifo kwa Khamenei,” huku wanafunzi wakikusanyika katika vyuo vikuu kadhaa.

FILE - Waandamanaji wakichoma pikipiki ya polisi wa maadili mjini Tehran, Iran Septemba 19, 2022.
FILE - Waandamanaji wakichoma pikipiki ya polisi wa maadili mjini Tehran, Iran Septemba 19, 2022.

Maafisa wa haki za binadamu wa UN wamelaani ukamataji wa kutumia nguvu unaofanywa na polisi wa Jamhuri ya Kiislam dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali ikiwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na wamezitaka mamlaka husika nchini Iran kusitisha ukamataji wa mabavu dhidi ya waandamanaji wa amani.

Maandamano hayo yalianza katikati ya mwezi Septemba baada ya kukamatwa na siku chache baadae kufariki Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22. Alikuwa anashikiliwa na polisi wa maadili wa Iran kwa kutojifunika inavyotakiwa nywele zake kutumia hijabu.

Mikaeil Alizadeh, anayejulikana kwa jina la Leo, akiwatumbuiza waandamanaji mjini Istanbul, Uturuki. October 4, 2022.
Mikaeil Alizadeh, anayejulikana kwa jina la Leo, akiwatumbuiza waandamanaji mjini Istanbul, Uturuki. October 4, 2022.

Kikundi cha Haki za Binadamu cha Iran kimesema wiki hii idadi ya vifo kutokana na msako unaoendelea dhidi ya waandamanaji nchi nzima vimefikia takriban 215, kati yao 27 ni watoto.

Serikali ya Iran imedai Amini alipata mshtuko wa moyo na hakuwa ametendewa vibaya. Familia yake ilisema alikuwa hana historia ya matatizo ya moyo na kuwa miwili wake ulikuwa na mikwaruzo na alama nyingine za kupigwa.

Wakati huo huo, raia wa nchi 144 wamekamatwa kuhusiana na maandamano katika wiki za hivi karibuni na utawala wa Iran, kituo cha habari ambacho kiko karibu na Jeshi la Ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislam (IRGC) kimeripoti Jumatano.

Ripoti hiyo imesema wale waliokamatwa ni pamoja na raia wa Marekani, Russia, Austria , Ufaransa, Uingereza na Afghanistan.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG