Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 19:34

Makombora zaidi ya Russia yaangushwa Kyiv huku wanajeshi wa Ukraine wakidhibiti tena sehemu za kusini


Picha inayoonyesha nyumba iliyoharibiwa kwa kombora, katika mji wa Kyiv, Ukraine. Picha hii ilitolewa na maafisa wa usalama wa Ukraine na ilipigwa kuwa kutumia ndege ndogo isiyokuwa na rubani.
Picha inayoonyesha nyumba iliyoharibiwa kwa kombora, katika mji wa Kyiv, Ukraine. Picha hii ilitolewa na maafisa wa usalama wa Ukraine na ilipigwa kuwa kutumia ndege ndogo isiyokuwa na rubani.

Wanajeshi wa Russia wameshambulia katikati ya mji wa Kyiv kwa makombora yanayorushwa na ndege zisizo na rubani, asubuhi na mapema Jumatatu, wakati watu walikuwa wanakwenda kazini.

Hii ni mara ya pili makombora ya Russia yanashambulia katikati mwa Kyiv, huku wanajeshi wa Russia wakiendelea kupoteza nguvu katika sehemu walizokuwa wameshikilia.

Wanajeshi wa Ukraine walijaribu kupiga ndege zisizo na rubani za Russia katikati mwa Kyiv.

Wakaazi wa Kyiv walikimbia wakitafuta pa kujificha.

Afisa katika ofisi ya rais wa Ukraine amesema kwamba watu watatu wamefariki kutokana na mashambulizi ya leo dhidi ya jengo linalokaliwa na watu mjini Kyiv.

Ndege zisizo na rubani ni za Iran

Ukraine imesemsa kwamba mashambulizi ya leo yametekelezwa na ndege zisizo na rubani zilizotengenezwa nchini Iran.

Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema kwamba imetekeleza mashambulizi “makubwa sana” dhidi ya kambi za kijeshi na miundo mbinu muhimu ya Ukraine kwa kutumia silaha nzito.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine Denys Monastyrskyi amesema kwamba kuna vifo vimeripotiwa katika miji mingine katika mashambulizi ya leo Jumatatu.

Mashambulizi ya leo yametokea wiki moja baada ya Russia kuangusha makombora kadhaa mjini Kyiv na miji mingine tangu vita vilipoanza nchini Ukrane. Mashambulizi hayo yalitekelezwa wakati idadi kubwa ya watu walikuwa wanaelekea kazini.

"Usiku mzima, asubuhi yote, adui amekuwa akishambulia raia. Makombora yanashambulia Ukraine nzima. Jengo linalokaliwa na watu limepigwa mjini Kyiv,” amesema rais wa Ukraine President Volodymyr Zelenskiy akiongezea kusema kwamba “adui anaweza kushambulia miji yetu lakini hatatumaliza nguvu. Wanaotuvamia wataadhibiwa na kuhukumiwa na jamii ijayo. Tutashinda.”

Jeshi la Ukraine limesema kwamba limeharibu makombora 37 (asilimia 85) yaliyorushwa na jeshi la Russia tangu Jumapili.

Madai ya Iran kusaidia Russia kushambulia Ukraine

Ndege isiyokuwa na abiria ikikaribia kutekeleza shambulizi mjini Kyiv, Ukraine Oct. 17, 2022.
Ndege isiyokuwa na abiria ikikaribia kutekeleza shambulizi mjini Kyiv, Ukraine Oct. 17, 2022.

Mkuu wa haki za kibinadamu katika Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema kwamba mashambulizi ya makombora dhidi ya raia lazima yakomeshwe.

Ubalozi wa Marekani mjini Kyiv umeshutumu mashambulizi hayo.

Iran imeendelea kukanusha ripoti kwamba inatoa msaada wa ndege zisizo na rubani kwa Russia.

Baadhi ya mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa ya Ulaya, wanaokutana Luxembourg, wametaka Iran kuwekewa vikwazo vipya iwapo madai ya Tehran kuisaidia Russia katika mashambulizi dhidi ya Ukraine yanathibitishwa.

Mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak amesema kwamba Russia inastahili kuondolewa kama mwanachama wa kundi la nchi 20 tajiri zaidi duniani na kutolewa pia katika miungano mingine ya nchi duniani, kutokana na mashambulizi yake dhidi ya Ukraine.

Russia imeshutumu Ukraine kwa kushambulia eneo la Belgorod, mpakani mwa nchi hizo mbili.

Vyombo vya habari nchini Russia vimeripoti kwamba wanajeshi wa Ukraine wameshambulia uwanja wa ndege wa Belgorod usiku wa kuamkia leo.

Hakuna taarifa imetolewa na Kyiv kuhusu madai hayo. Utawala wa Kyiv huwa hauzungumzi kuhusu maswala yanayoendelea ndani ya Russia.

Mashambulizi karibu na kinu cha Nyuklia

Kinu cha Nyuklia cha Zaporizhzhia kinachotengeneza nguvu za umeme, Enerhodar, Zaporizhzhia kusini mwa Ukraine, on May 1, 2022.
Kinu cha Nyuklia cha Zaporizhzhia kinachotengeneza nguvu za umeme, Enerhodar, Zaporizhzhia kusini mwa Ukraine, on May 1, 2022.

Mashambulizi ya Russia yametokea karibu na kinu cha Nyuklia cha Zaporizhzhia ambapo ni kiwanda kikubwa zaidi ya Nyuklia Ulaya.

Mashambulizi hayo yamepelekea kiwanda hicho kuzimwa na kusababisha ukosefu wa umeme.

Kiwanda cha Nyuklia cha Zaporizhzhia kinashikiliwa na wanajeshi wa Russia lakini wafanyakazi wake ni raia wa Ukraine. kimekuwa kikishambuliwa kila mara.

Russia inakabiliwa na changamoto nyingi

Ujasuri wa serikali ya Uingereza umesema kwamba wanajeshi wa Russia wanakabiliwa na wakati mgumu tangu daraja linalounganishwa Russia na Crimea kuharibiwa katika shambulizi la Oktoba 8.

Mapigano makali yanaendelea katika mji wa Bkhmut na katika mji wa Soledar.

Mji wa Bakhmut umekuwa lengo kubwa la wanajeshi wa Russia kuelekea eneo la Donetsk tangu walipodhibithi miji ya viwanda ya Lysychansk na Sievierodonetsk mwezi June na July.

Mji wa Soledar unapatikana kaskazini mwa Bakhmut.

Mataifa ya magharibi yamekuwa yakitoa msaada wa silaha kwa wanajeshi wa Ukraine kuendelea kupambana na wanajeshi wa Russia.

Wanajeshi wa Ukraine wanaendelea kukomboa sehemu za nchi

wanajeshi wa Ukraine wakitekeleza mashambulizi katika eneo la Kharkiv, Ukraine, Oct. 5, 2022.
wanajeshi wa Ukraine wakitekeleza mashambulizi katika eneo la Kharkiv, Ukraine, Oct. 5, 2022.

Wanajeshi wa Ukraine wamefanikiwa kuwafukuza wanajeshi wa Russia na kudhibithi sehemu ya kusini mwa eneo la Kherson ambayo inaunganisha Crimea na sehemu zingine za Ukraine.

Wamedhibithi pia sehemu za kaskazini mashariki baada ya mapigano makali ya miwezi miwili.

Mafanikio ya wanajeshi wa Ukraine yamepelekea rais wa Russia Vladimir Putin kutangaza kusajiliwa kwa wanajeshi wa akiba 300,000, ikiwa ni hatua huwani kuchukuliwa na Russia tangu kutokwa kwa vita vya pili vya dunia.

Wanaumme wengi wa Russia walikimbilia nchi Jirani kufuatia tangazo la Putin la kusajili wanajeshi 300,000 kwa ajili ya vita nchini Ukraine.

XS
SM
MD
LG