Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 04:58

Russia imekimbilia Iran na Korea kaskazini kwa msaada wa silaha, vikwazo dhidi ya Iran vinajadiliwa


Wanajeshi wa Ukraine wakikusanya makombora ya Russia katika kijiji cha Berezivka, Ukriane, Aprili 21,2022
Wanajeshi wa Ukraine wakikusanya makombora ya Russia katika kijiji cha Berezivka, Ukriane, Aprili 21,2022

Iran imeahidi kuipatia Russia makombora Pamoja na ndege zisizo na rubani, kwa ajili ya mashambulizi yake dhidi ya Ukraine.

Shirika la habari la Reuters linaripoti kwamba maafisa wa ngazi ya juu wa Iran, wamesema hayo.

Makubaliano ya ununuzi wa makombora hayo ulifanyika Oktoba 6, wakati makam wa kwanza war ais wa Iran Mohammad Mokhber, maafisa wawili wa ngazi ya juu wa kikosi cha ulinzi cha Iran na afisa kutoka baraza la ngazi ya juu kabisa la usalama wa Iran walipokutana mjini Moscow kwa mazungumzo na maafisa wa Russia kuhusu usafirishaji wa silaha.

"Russia imeomba ndege zisizokuwa na rubani Pamoja na makombora ya masafa marefu ya Iran, yenye uwezo mkubwa wa kulenga shabaha,” amesema afisa wa kidiplomasia wa Iran.

Mojawapo ya silaha ambazo Iran imekubali kuipa Russia ni ndege isiyo na rubani aina ya Shahed -136, inayojulikana kama Kamikaze. Inabeba silaha zenye uwezo wa kulenga shabaha na kutekeleza uharibifu mkubwa.

Makombora ya Iran ya Fateh-110 na Zolfaghar ya masafa mafupi pia ni kati ya silaha ambazo Russia imeomba Iran. Yana uwezo wa kutekeleza mashambulizi umbali wa hadi kilomita 700.

Mkataba wa usalama wa umoja wa mataifa

Silaha za vita za Iran
Silaha za vita za Iran

Iran imesema kwamba makubaliano yake ya silaha na Russia hayavunji kanuni za usalama la umoja wa mataifa za mwaka 2015.

"Mahali silaha hizi zinatumika sio swala la muuzaji kujua. Hatuhusiki katika vita vya Ukraine namna yanavyofanya mataifa ya magharibi. Tunataka kumaliza hivi vita kupitia njia ya kidiplomasia,” amesema mwanadiplomasia wa Iran.

Ukraine imeripoti kuongezeka kwa mashambulizi ya makombora yanayotekelezwa na wanajeshi wa Russia wakitumia makombora ya Iran.

Wizara ya mambo ya nje ya Iran imefutilia mbali ripoti kwamba Iran inatoa silaha kwa Russia kutumika katika vita vya Ukraine, huku Russia ikifutilia mbali ripoti kwamba inatumia ndege zisizo na rubani za Iran kushambulia Ukraine.

Usafirishaji wa silaha kutoka Iran hadi Russia kufanyika hivi karibuni

Mkuu wa kikosi cha jeshila mapinduzi la Iran Generali Hossein Salami
Mkuu wa kikosi cha jeshila mapinduzi la Iran Generali Hossein Salami

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema kwamba ndege zisizo na rubani za Iran zilitumika kutekeleza mashambulizi ya makombora mjini Kyiv, Ukraine saa za asubuhi wakati watu walikuwa wanaelekea kazini.

Msemaji wa white house Karinne Jean-Pierre ameshutumu Tehran kwa kusema uongo kwamba ndege zisizo na rubani za Iran hazitumiki katika vita vya Ukraine.

Mwanadiplomasia wa Umoja wa ulaya amesema kwamba Russia inakumbana na wakati mgumu kutengeneza silaha zake kutokana na vikwazo vilivyowekewa sekta yake ya viwanda na hivyo inatafuta msaada kutoka kwa washirika wake ambao ni Iran na Korea kaskazini.

Kamanda wa jeshi la mapinduzi la Iran Hossein Salami, alisema mwezi uliopita kwamba “nchi zenye nguvu duniani zinataka kununua silaha na vifaa vya ulinzi kutoka kwa Iran”,

Rahim Safavi, mshauri wa kiongozi wa juu kabisa wa Iran, alinukuliwa na shirika la habari la serikali ya Iran jumanne, akisema kwamba nchi 22 zinataka kununua ndege zisizokuwa na rubani za Iran.

“siwezi kusema muda maalum silaha zitasafirishwa, lakini hilo litafanyika hivi karibuni. Meli mbili au tatu zitasafirisha silaha hizo,” amesema afisa wa ngazi ya juu wa Iran.

Vikwazo dhidi ya Iran

Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Nchi kadhaa za umoja wa ulaya zinataka Iran kuwekewa vikwazo kutokana na hatua yake ya kutoa silaha kwa Russia.

Iran inakabiliwa na maandamano makubwa ndani ya nchi kufuatia kifo cha mwanamke aliyefariki akiwa mikononi mwa polisi baada ya kukamatwa kwa kukosa kufunika kichwa.

Mataifa ya magharibi yanataka Iran kuwekewa vikwazo kwa kukandamiza waandamanaji.

Iran inakabiliwa na wakati mgumu, inapojaribu kufufua mazungumzo ya mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 kw alengo la kutaka vikwazo dhidi yake kulegezwa.

Mazungumzo ya nyuklia yalikwama na mgogoro wa aina yoyote kati ya Iran na mataifa ya magharibi unaweza kuharibu zaidi mazungumzo hayo.

Marekani imekubaliana na ripoti ya Uingereza na Ufaransa kwamba Iran inatoa ndoa zisizo na rubani kwa Russia, na kwamba hatua hiyo inavunja mkataba wa mwaka 2015 wa baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Mnamo mwezi Septemba, Tehran ilikataa ombi la rais wa Russia Vladimir Putin la kutaka kupewa ndege zisizokuwa na rubani, senye uwezo wa kulenga shabaha kwa masafa marefu.

XS
SM
MD
LG