Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 19:11

Umoja wa Ulaya umewawekea vikwazo maafisa wa polisi wa maadili wa Iran


Bendera za Muungano wa Ulaya zinapepea nje ya makao makuu ya Tume ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji Juni 17, 2022. REUTERS.
Bendera za Muungano wa Ulaya zinapepea nje ya makao makuu ya Tume ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji Juni 17, 2022. REUTERS.

Umoja wa Ulaya Jumatatu umewawekea vikwazo maafisa wa polisi wa maadili wa Iran na waziri wa habari wa Tehran kwa jukumu lao katika ukandamizaji mkali wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya waandamanaji.

Waandamanaji hawa walikuwa wanapinga kifo cha msichana aliyeshikiliwa na polisi wa maadili kwa kushindwa kufunika nywele zake vizuri na hijabu.

Jumuiya hiyo yenye nchi 27 ilizuia mali za watu 11, wakiwemo maafisa wawili wakuu wa polisi wa maadili, Mohammad Rostami na Haj Ahmad Mirzaei, na Waziri wa Habari Issa Zarepour, ambaye alitajwa kuhusika katika kuzima mtandao baada ya maandamano kuanza. Pia walipigwa marufuku kusafiri Ulaya.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, waliokutana Luxembourg, pia walilenga Vikosi vya Utekelezaji Sheria vya Iran na wakuu kadhaa wa polisi wa eneo hilo kwa jukumu lao katika ukandamizaji wa kikatili wa maandamano.

Maandamano hayo yalianza katikati ya mwezi Septemba baada ya kukamatwa na kufariki siku chache baadaye kwa Mahsa Amini, ambaye alikuwa na umri wa miaka 22. Darzeni ya waandamanaji wameuawa na maafisa usalama wakati wa maandamano mitaani kote nchini Iran.

XS
SM
MD
LG