Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 16:20

Maandamano kuadhimisha kumbukumbu ya umwagaji damu wa mwaka 2019 yafanyika miji mbalimbali ya Iran


FILE - Kundi la waandamanaji wakipiga makelele matamko ya hasira mbele ya mlango mkuu wa eneo kuu la soko la biashara la Grand Bazaar mjini Tehran, Iran.
FILE - Kundi la waandamanaji wakipiga makelele matamko ya hasira mbele ya mlango mkuu wa eneo kuu la soko la biashara la Grand Bazaar mjini Tehran, Iran.

Wananchi wa Iran wako katika mgomo katika miji kadhaa nchini  humo siku ya Jumanne ikiwa ni kumbukumbu ya  maandamano ya kupinga ongezeko la bei ya mafuta mwaka 2019.

Maandamano hayo yalikuwa ni upinzani wa wazi ambao ulikabiliwa na majeshi ya usalama katika msako mkali uliokuwa na umwagaji wa damu katika historia ya Jamhuri ya Kiislam.

Mgomo huo utaongeza shinikizo kwa viongozi wa kidini wa Iran, ambao wamekuwa wakipambana kwa miezi miwili na maandamano ya nchi nzima yaliyochochewa na kifo cha msichana wa Kikurdi Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22 aliyefariki akiwa chini ya ulinzi wa polisi wa maadili.


Mwaka 2019, Reuters iliripoti watu 1,500 waliuawa katika wimbi la ghasia lililoanza kutokana na ongezeko la bei ya mafuta lakini mara likageuka kuwa la kisiasa. Mamlaka nchini Iran zilikanusha idadi hiyo ya vifo.

Katika maandamano ya karibuni, shirika habari la wanaharakati wa haki za binadamu (HRANA) lilisema kuwa watu 344 wameuawa, ikiwemo watoto 52. Pia imeripoti wanajeshi 40 wa vikosi vya usalama wameuawa, ikiwa ni pamoja na watu 15,820 waliokamatwa.

Maandamano hayo yamegeuka kuwa ni mgogoro halali kwa utawala wa kidini, ambao ulichukua madaraka baada ya mapinduzi ya mwaka 1979 yaliyomuondoa madarakani Shah Mohammad Reza Pahlavi, kiongozi wa utawala wa kifalme uiokuwa haukuelemea katika dini na mafungamano na nchi za Magharibi.

Picha za Video zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zilionyesha mashambulizi na mikusanyiko mbalimbali katika miji kadhaa na majiji mbalimbali. Pia picha zilizosambazwa na wanaharakati ambao akaunti yao ya mtandao wao wa Twitter 1500Tasvir uliokuwa na wafuasi sehemu mbalimbali zilionyesha maduka yamefungwa katika eneo kuu la biashara la Grand Bazaar mjini Tehran. Video moja, ambayo haikuthibitishwa na Reuters, ilionyesha wenye maduka wakipiga kelele: “Huu ni mwaka wa umwagaji damu wakati (Kiongozi Mkuu wa Kidini Ayatollah Ali) Khamenei atakapopinduliwa.”

Wafanyabiashara eneo la Bazaar kwa kawaida ni washirika wakuu kabisa wa kifedha wa serikali ya kidini.

Shirika la habari la serikali ya Iran IRNA limethibitisha mgomo wa wafanyabiashara katika soko la Bazaar mjini Tehran, lakini limesema wafanyabiashara walilazimishwa na “wafanya ghasia” kufunga maduka yao.

Wakikaidi wito wa viongozi wa Magharibi na vikundi vya kutetea haki kumaliza ukamataji kwa waandamanaji, mahakama ya Mapinduzi nchini Iran imemhukumu mwandamanaji adhabu ya kifo Jumanne.

Shirika la habari la mahakama Mizan lilisema “mfanya ghasia alihukumiwa adhabu ya kifo kwa kosa la ‘moharebeh’ (kuanzisha vita dhidi ya amri ya Mungu) kwa kutumia kisu kutishia wengine,” ikiongeza kuwa anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Muandamanaji mwingine alihukumiwa kifo kwa kuwasha moto jengo la serikali, vyombo vya habari vya serikali vilieza mahakama ikieleza hilo Jumapili.

Watu wapatao 19 kati ya maelfu waliokamatwa wanakabiliwa na mashtaka yenye adhabu ya kifo katika miji kadhaa ya Tehran na jirani yake wa Karaj, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya serikali.

XS
SM
MD
LG