Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 23:50

Ahukumiwa kifo kwa kuandamana Iran


Serikali ya kimapinduzi ya Iran imetoa hukumu ya kifo kwa mwandamanaji mmoja aliyekuwa akikosoa serekali, na wengine watano kupewa hukumu ya kwenda gerezani.

Shirika la habari la serikali, limeripoti hayo Jumapili wakati ambapo bado hakuna hali ya utulivu nchini humo.

Hukumu hiyo inafanya kuwa ya kwanza ya kifo katika kesi zinazo husiana na wale waliokamatwa kwa kushiriki maandamano ambayo yamefanyika kote Iran katika wiki kadhaa zilizopita yakitaka kumalizwa kwa utawala wa kiimla.

Mtandao wa Mizan wenye uhusiano na idara ya mahakama ya Iran, umeeleza hukumu ya kifo inatokana na mashitaka ya waandamanaji kuwasha moto katika majengo ya serekali.

Hukumu za kwenda gerezani zilizo tolewa zinaanzia miaka mitano mpaka kumi kwa mashitaka ya kukiuka sheria za usalama wa taifa na kukiuka amri.

Maandamano yameingia wiki ya nane na yalizuka baada ya kifo cha binti wa miaka 22 Mahsa Amini aliyekuwa akishikiliwa

XS
SM
MD
LG