Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 12:23

Takriban watu 1000 washtakiwa kwa kuandamana Iran


Iran inaendelea kukabiliwa na machafuko ya nchi nzima yaliyotokana na kifo cha Septemba 16 cha Amini. (AP)

Uongozi wa Kidini nchini Iran umejibu kutokana na maandamano ya wiki kadhaa na ukandamizaji ambao, zaidi ya kuua dazeni, pia umepelekea watu 1,000 kushtakiwa hadi sasa katika mfumo wa mahakama usio wa wazi.

Ripoti kutoka Iran zinasema waandamanaji hao kwa mara nyingine tena walipambana na vikosi vya usalama Alhamisi katika eneo lililo karibu na mji mkuu, wakiripotiwa kuwaua au kuwajeruhi wanachama wa vikosi vya usalama.

Maandamano nchini Iran yamezuka karibu kila siku tangu Septemba baada ya kifo cha Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22 akiwa chini ya ulinzi wa Polisi wa maadili wa nchi hiyo.

Wachambuzi wanasema maandamano ya kila siku yamekuwa baadhi ya changamoto kubwa kwa Jamhuri hiyo ya Kiislamu katika historia yake.

Mapigano ya Alhamisi yalikuja baada ya maelfu ya watu kukusanyika katika mji wa Karaj, nje kidogo ya Tehran, kuadhimisha siku ya 40 tangu kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Hadis Najafi mwenye umri wa miaka 22, mmoja wa wanawake vijana kadhaa waliouawa wakati wa maandamano

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG