Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 01:54

Waandamanji Iran waadhimisha siku 40 tangu mauwaji ya Zahedan.


Maandamano nchini Iran
Maandamano nchini Iran

Shirika la kutetea haki za binadamu lenye makao yake Norway, limeeleza kuwa, miji mbali mbali Magharibi mwa Iran yamefanya migomo ikiwa ni mshikamano kwa waombolezaji waliokuwa wakiadhimisha siku 40 tangu maafisa wa usalama walipouwa darzeni ya watu huko Zahedan.

Vikosi vya usalama viliwashambulia waandamanji hapo Septemba 30, baada ya sala ya ijumaa mjini Zahedan, mji mkuu wa jimbo la Sistan Baluchistan, kusini mashariki mwa mpaka na Pakistan.

Msako huo ulitokea wiki mbili baada ya maandamano kufanyika kote nchini Iran kufuatia kifo cha Mahsa Amini, msichana wa kikurdi mwenye umri wa miaka 22 alipokamatwa kwa kukiuka kanuni za nchi hiyo zinazoagiza wanawake kuvaa hijab. Mahsa Amini baadaye alifariki akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Maandamano makubwa yalifanyika leo Jumatano katika miji ya Magharibi ya Kikurdi ya Baneh, Kermanshah, Marivan,Sanandaj na mji wa Saqez, ambako anatokea Mahsa Amini.

Shirika la haki za binadamu la Hengaw, limeeleza kuwa maandamano yalifanyika wakiadhimisha siku 40 tangu vifo vilivyotokea huko Zahedan.

Ghasia zilizoibuka huko Zahedan hapo September 30, zilichochewa na ubakaji wa msichana mwenye umri wa miaka 15, uliofanywa na kamanda mmoja wa polisi katika mji wa bandari wa Chabahar.

Vikosi vya usalama waliwashambulia watu waliofurika mitaani baada ya kumaliza sala za Ijumaa, na kupelekea dazeni ya watu kuuwawa .

Shirika la Hengaw, linasema kuwa kile kilichofanyika siku hiyo ya Ijumaa huko Zahedan, kulingana na sheria za kimataifa, ni dhahiri mauaji ya raia wengi, na shirika hilo linataka mauaji hayo yatambuliwe na mashirika ya kimataifa na serikali za Magharibi.

Watu takriban 118 waliuwawa katika jimbo la Sistan Baluchistan, na Maafisa wa serikali ya Iran nao wanasema kuwa maafisa wao wa usalama takriban 6 nao wameuwawa.

Zahedan, ni mojawapo ya miji michache yenye wafuasi wengi wa dhehebu la sunni, katika taifa ambalo waumini wake wengi ni kutoka dhehebu la shia.

XS
SM
MD
LG