Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 02:40

Maafisa : Vifo vya tembo Botswana vilisababishwa na maji yenye sumu


Tembo katika hifadhi ya wanyama Botswana

Vifo vya mamia ya tembo nchini Bostwana mwaka 2020 vimewashangaza na kuwatia wasi wasi mkubwa watalaamu wa hifadhi, vimesababishwa na sumu iliyokuwepo kwenye maji, maafisa wamesema Jumatatu. 

Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyama Pori na Hifadhi za Taifa, Cyril Taolo ameuambia mkutano wa waandishi wa habari idadi ya tembo waliokufa imepanda na kufikia 330, kutoka 281 walioripotiwa mwezi Julai.

Afisa wa Wanyama katika idara hiyo, Mmadi Reuben amesema kwamba hata hivyo bado kuna maswali ambayo hayajajibiwa.

Botswana ina kiasi cha theluthi moja ya idadi ya tembo barani Afrika, kiasi cha 130,000.

Majangili hawajahusishwa kuwa moja ya sababu ya vifo vya tembo kwa sababu mizoga yao inakuwa haijaguswa hata kidogo.

Uchunguzi wa awali ulianzishwa baada ya kundi la Elephants Without Borders EWB kuripoti vifo wakati wa utafiti wao wa angani.

Wakati huo, mkurugenzi wa EWB, Mike Chase alisema tembo wengi walionekana kuwa ni dhaifu na wamekonda sana.

Baadhi ya tembo walionekana kushindwa kutembea, walionyesha dalili za kupooza au kuchechemea, amesema Chase.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG