Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 11, 2024 Local time: 06:33

Kifo cha Ginsburg kinaweza kupelekea majaji wa mrengo wa kulia kuidhibiti Mahakama ya Juu


FILE - Marehemu Ruth Bader Ginsburg
FILE - Marehemu Ruth Bader Ginsburg

Kifo cha Jaji mwenye msimamo wa kiliberali katika Mahakama ya Juu Marekani, Ruth Bader Ginsburg kinampa fursa Rais Donald Trump kuongeza jaji Mconservative katika jopo la mahakama na kuhamisha uwiano wa itikadi ya mahakama ya juu yenye nguvu upande wa mrengo wa kulia. 

Ikiwa na majaji waliowengi zaidi katika jopo hilo, masuala mengi kwa upana zaidi yanaweza kuathirika. Wateule wengine wa Trump wa Mahakama ya Juu – majaji waconservative Neil Gorsuch na Brett Kavanaugh – walikuwa wamewarithi majaji wengine waliokuwa wameteuliwa na marais Warepublikan.

Hivi sasa kufuatia kifo cha Ginsburg, Trump anaweza kufanya kitu ambacho hakuna rais mwengine alitekeleza katika kizazi kilichopita: kumweka jaji mconservative nafasi iliyoachwa wazi na jaji mliberali.

Mara ya mwisho fursa hii ilitokea ni wakati Rais mrepublikan George H.W Bush alipomteua jaji mconservative Clarence Thomas mwaka 1991 kumrithi mliberali maarufu Thurgood Marshall katika mahakama hiyo.

Rais Donald Trump akitoa rambirambi juu ya kifo cha Jaji Ruth Bader Ginsburg baada ya kampeni yake uwanja wa ndege wa Bemidji Airport, Bemidji, Minnesota, Sept. 18, 2020.
Rais Donald Trump akitoa rambirambi juu ya kifo cha Jaji Ruth Bader Ginsburg baada ya kampeni yake uwanja wa ndege wa Bemidji Airport, Bemidji, Minnesota, Sept. 18, 2020.

Ginsburg aliteuliwa kuingia Mahakama ya Juu mwaka 1993, alifariki nyumbani kwake Washington Ijumaa akiwa na umri wa miaka 87 baada ya kuugua saratani mara tano, alikuwa ndiye mtu mzima zaidi na aliyehudumu muda mrefu kama jaji mliberali katika Mahakama ya Juu ambayo kwa kawaida ina majaji tisa

Kwa miezi kadhaa, wakati Afya ya Ginsburg ikiendelea kuwa mbaya, waliberali walikuwa na wasiwasi kuwa kifo chake kitamwezesha Trump kumchagua mrithi wake kabla ya uchaguzi wa mwezi Novemba na haijalishi iwapo wapiga kura watamchagua Trump kwa mara nyingine kuongoza kwa awamu ya pili.

Kwa waliberali wengi, hofu yao kubwa zaidi imefikiwa. “Mteule anayefuata bila shaka ni yule mwenye mrengo wa kulia” kama Kavanaugh na Gorsuch, wateule wawili wa Trump katika Mahakama ya Juu, amesema Gabe Roth, mkurugenzi mtendaji wa mrengo wa kushoto katika muungano wa uwazi katika mahakama.

Mtetezi wa haki za wanawake wakati wa uhai wake, Ginsburg aliwahi kuhudumu katika nafasi ya jaji wa serikali kuu kutoka mwaka 1980 hadi 1993 na hapo Rais Bill Clinton alimteua kuingia Mahakama ya Juu na kuwa mwanamke pekee wa pili katika historia kutumikia katika jopo hilo.

Rais mstaafu Bill Clinton
Rais mstaafu Bill Clinton

Kabla ya kuwa jaji wa serikali kuu, Ginsburg aliacha alama kama mtetezi wa haki za wanawake katika jumuia ya kupigania uhuru wa kiraia katika miaka ya 1970, akiongoza kesi kubwa dhidi ya ubaguzi wa jinsia.

Kama anavyojulikana kwa kusema ukweli, alitofautiana wazi wazi na Trump wakati wa kampeni yake ya urais 2016, akimwita “mdanganyifu” iliyopelekea tajiri huyo wa biashara ya majumba kumtaka ajiuzulu.

Katika taarifa yake aliyoitoa Ijumaa jioni, Trump alimpongeza Ginsburg kama “mpiganaji,” akisema maoni yake ya kisheria “yaliwahamasisha Wamarekani wote na vizazi kadhaa vyenye ufahamu bora wa sheria.”

“Nina mabinti wanne, na niliwaambia hivi sasa kuwa mwanamke huyu peke yake aliweza kuanzisha haki za wanawake kuwafanya wawe sawa na binadamu yeyote,” amesema Kimberly Wehle, mhadhiri wa sheria katika Chuo Kikuu cha Baltimore.

Bila shaka kuna wanawake kadha wa kadha na wanaume waliochangia katika hilo. Lakini kwa namna sheria ilivyo uundwa, ilikuwa ni kazi yake kama wakili na bila shaka kama jaji wa Mahakama ya Juu.

Kufuatia kifo cha Ginsburg, Mahakama ya Juu kiitikadi imegawanyika kati ya waconservative watano – wakiwemo wateule wawili wa Trump – na waliberali watatu. Jaji Mkuu Mconservative John Roberts baadhi ya nyakati amekuwa akihama katika kura yake.

Kuongezeka kwa jaji mconservative wa sita itawapa nguvu kile waconservative walichokuwa wanakiona udhaifu wa kuweza kuidhibiti mahakama hiyo.

“Inaleta tofauti kubwa iwapo una majaji wenye msimamo wa kiconservative sita katika mahakama hiyo au majaji watano waconservative katika Mahakama hiyo,” John Malcolm, Makamu wa Rais wa taasisi ya Serikali ya Kikatiba katika Taasisi ya Conservative Heritage Foundation amesema.

Taasisi ya Heritage Foundation na Jumuiya ya Conservative Federalist wote wameishauri White House juu ya wateule wa Trump katika mahakama.

Gorsuch na Kavanaugh – wakati wote ni Waconservative – baadhi ya wakati wametofautiana na wenzao na kupiga kura na Waliberali katika masuala muhimu.

FILE - Majaji wa Mahakama ya Juu Neil Gorsuch, kushoto, na Brett Kavanaugh
FILE - Majaji wa Mahakama ya Juu Neil Gorsuch, kushoto, na Brett Kavanaugh

Trump ambaye katika kampeni yake alisema atawateua majaji waconservative miaka minne iliyopita na anaona fahari kwa rekodi yake ya uteuzi wa mahakama, hivi karibuni alitoa orodha ya wateule 20 wenye sifa za kuingia Mahakama ya Juu, akiwaelezea kuwa ni majaji walioandaliwa kwa mfano wa marehemu Jaji wa Mahakama ya Juu Antonin Scalia na majaji waconservative wa hivi sasa Clarence Thomas na Samuel Alito.

Kati ya wale wanaopendekezwa zaidi katika orodha ya Trump ni Amy Coney Barrett, Amul Thapar na Thomas Hardiman, wote hivi sasa ni majaji wa mahakama ya rufaa.

Iwapo Trump ataamua kumteua mwanamke kuwa mrithi wa Ginsburg, kuna uwezekano mkubwa Barret atapewa kipaumbele, Malcolm amesema.

Barrett, miaka 48, aliteuliwa katika mahakama ya rufani ya serikali kuu kwa wilaya ya saba mwaka 2017.

Malcolm amemuelezea mwanamke huyu kama ni muumini wa kufasiri sheria kama ilivyoandikwa na kufuata asili yake – nadharia za kutafsiri nadharia zilizoanzishwa na waconservative.

“Nitasema hivyo hivyo juu ya kila mmoja ambaye yuko kwenye orodha ya Trump,” amesema Malcolm.

Wehle, ambaye ni mwandishi wa kitabu juu ya Katiba ya Marekani, alisema uteuzi wa jaji mconservative mwengine kunaweza kuathiri masuala yenye utata kadhaa : haki ya kutoa mimba, uhamiaji, huduma ya afya, kutenganisha kanisa na serikali na mengineyo.

“Inahitaji theluthi mbili ya waliowengi kwa mabaraza yote ya Bunge la Marekani na kupitishwa kwa theluthi tatu kwa majimbo yote kurekebisha Katiba kwa matakwa ya wananchi,” Wehle amesema.

“Lakini inahitaji majaji watano wa kudumu katika Mahakama ya Juu ya Marekani kubadilisha Katiba katika uamuzi wao.”

Rais Donald Trump (kulia) akizungumza na kiongozi wa waliowengi Baraza la Seneti Mitch McConnell White House in Washington, Julai 20, 2020.
Rais Donald Trump (kulia) akizungumza na kiongozi wa waliowengi Baraza la Seneti Mitch McConnell White House in Washington, Julai 20, 2020.

Matarajio mema ni kwamba Trump ataweza kumteua jaji mconservative kumrithi Ginsburg, hata kama atashindwa katika uchaguzi wa Novemba na mpinzani wake Joe Biden.

Kwa msaada wa kiongozi wa waliowengi katika Baraza la Seneti Mitch McConnell wa Kentucky, Trump anaweza kujaribu kusukuma kupitishwa uteuzi wake kabla ya uchaguzi au – inawezekana zaidi – katika kikao ambacho bado wana nguvu Bungeni baada ya uchaguzi.

XS
SM
MD
LG