Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 22:55

Biden aendelea kuongoza katika kura za maoni Marekani


Makamu rais wa zamani wa Marekani na mgombea urais wa mwaka wa 2020 Joe Biden
Makamu rais wa zamani wa Marekani na mgombea urais wa mwaka wa 2020 Joe Biden

Ikiwa imebaki chini ya miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa Marekani ukusanyaji wa maoni unaonyesha mgombea kiti cha urais wa chama cha Demokratik bado anaongoza katika taifa zima na kuisababisha kampeni ya Rais Trump kuongeza juhudi zao katika majimbo yenye ushindani.

Huku wachambuzi wakisema masuala muhimu katika kampeni ya mwaka huu yatahusu utendaji kazi wa Rais Trump; hasa kuhusu suala la ugonjwa wa COVID19, hali ya uchumi, ubaguzi wa rangi na ukosefu wa ajira.

Rais Donald Trump akiongea na wafuasi wake mara baada ya kuwasili Wilmington
Rais Donald Trump akiongea na wafuasi wake mara baada ya kuwasili Wilmington

Kulingana na matokeo ya uchunguzi wa maoni uliotolewa mwishoni mwa wiki na mashirika mbali mbali ya habari yanaonyesha Biden yungali anaongoza kitaifa kwa asilimia 50 dhidi ya asilimia 46 alizonazo Rais Trump.

Hata hivyo uchunguzi umebaini kwamba Trump ameweza kupata nguvu katika majimbo yenye ushindani kama vile Pensylvania ambako Biden alikuwa akiongoza kwa karibu asilimia 10 na hivi sasa anaongoza kwa asilimia 4 tu kutokana na kampeni ya vitisho inayongozwa na Trump hasa suala la ubaguzi wa rangi kama mvutano unao shuhudiwa katika jimbo la Oregon na kwengineko nchini.

Polisi wakitumia kemikali za kusababisha mwili kuwasha na vizuizi kuwatawanya waandamanaji huko Portland, Oregon, Jumamosi Septemba 5, 2020
Polisi wakitumia kemikali za kusababisha mwili kuwasha na vizuizi kuwatawanya waandamanaji huko Portland, Oregon, Jumamosi Septemba 5, 2020

Kwa siku ya 100 sasa wanaharakati wamekuwa wakiandamana na kuzuka ghasia kati ya wafuasi wa vuguvugu la Black lives matter wanaotaka mageuzi katika mfumo wa sheria, polisi na kukomeshwa ubaguzi wa rangi na wafuasi wa mrengo mkali wa kulia.

Polisi mjini Porland waliwakamata darzeni ya waandamani mwishoni mwa wiki baada ya ghasia hizo kuzuka Ikiwa ni zaidi ya siku 100 tangu kuuwawa kwa Mmarekani Mweusi George Blake akiwa anashikiliwa na polisi.

Katika mji wa Rochester New York kulikuwepo pia na ghasia kufuatia habari za kuuliwa kwa Mmarekani Mweusi mwngine Daniel Prude tarehe 30 March. Mwanasheria mkuu wa New York ametangaza baraza la mahakimu kuchunguza kesi hiyo na Meya wa Rochester Lovely Warren ameunga mkono maandamano ya amani na kulaani ghasia.

Warren Meya wa Rochester New York anasema : "Ni jukumu langu kama meya wa mji huu kupatia heshima Maisha ya Bw Prude, na kutoruhusu kifo chake kuwa jambo lisilo na maana. Na hivyo nitafanya kila niwezalo kuleta mabadiliko katika namna polisi wanavyofanya kazi katika mji wetu ili kuwalinda na kuwatumkia wakazi wake."

Suala la mageuzi katika vikosi vya usalama limechukua nafasi ya juu katika kampeni za pande zote na Joe Biden anaezungumza zaidi na waandishi Habari hadi sasa anasema atafanya mageuzi hayo huku akimkosoa zaidi mpinzani wake Trump kwa kushindwa kupambana na janga la Corona na uchumi.

Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden akizungumza na waumini wa kanisa la Grace Lutheran Church, Kenosha, Wis., Thursday, Sept. 3, 2020. (AP Photo/Carolyn Kaster)
Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden akizungumza na waumini wa kanisa la Grace Lutheran Church, Kenosha, Wis., Thursday, Sept. 3, 2020. (AP Photo/Carolyn Kaster)

Joe Biden anasema : "Wakati wa janga hili kiwango cha ukosefu wa ajira kimekua kikipanda huku mataifa mengine viwango vimeongezeka kwa nusu tu. Ni kwa nini? Kwa sababu Rais amevuruga vibaya namna ya kukabiliana na Covid.

Naye Rais Trump akitumia jukwa la kuzungumzia corona na waandishi wa habari kutoka White House kuzungumzia masuala mbali mbali ya kampeni mwishoni mwa wiki amerudia tena wazo kwamba chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 itapatikana kabla ya mwisho wa mwaka.

Donald Trump anasema : "Tunaendelea vyema na kazi ya kutoa chanjo ifikapo mwisho wa mwaka na pengine hata kabla ya Novemba mosi. Tuna dhani huenda ikawa tayari hapa mwezi wa Oktoba na kampuni ya Pfizer ni miongoni mwa kampuni zinazoongoza.

Waatalamu wanapinga wazo hilo wakisema hakuna chanjo salama inayoweza kupatikana mwaka 2020.

XS
SM
MD
LG