Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 22:22

Biden asema kufunguliwa shule ni dharura ya kitaifa


Joe Biden

Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Demokrat Joe Biden Jumatano wakati akizungumza akiwa nyumbani kwake mjini Wilmington Delaware ameelezea wasiwasi wake kuhusiana na suala la kufunguliwa shule na anataka tahadhari ichukuliwe kuhakikisha usalama wao.

Pia Biden alijibu maswali kuhusu ziara aliopanga kuelekea mjini Kenosha Wisconsin kulikotokea maandamano siku kadhaa zilizopita huku akishambulia utawala wa Trump kutokana na ulivyoshughulikia janga la corona.

Amesema pia kufunguliwa kwa shule ni suala la dharura ya kitaifa na kwamba nia yake ya kutembelea mji wa Kenosha ni kuwaleta watu pamoja.

Biden anautembelea mji huo Alhamisi ambao hivi karibuni umeshuhudia maandamano makubwa na ghasia kupinga ukatili wa polisi akisema kuwa nia yake ni kuleta afweni baada ya ziara ya rais Trump iliyopingwa na wakuu wa mji hapo Jumanne.

Biden amesema kuwa ziara yake ni ya kuhakikisha kuwa “sote tunasonga mbele” alipokuwa anazungumza na waandishi habari kutoka nyumbani kwake Wilmington Delaware.

Biden, Mgombea Urais Demokrat anafafanua : "Kumekuwa na shinikizo kubwa kwamba nitembelee mji huo kwa kuwa kinachohitajika ni uponyaji pamoja na kuwaleta watu pamoja. Nia yangu ya kutembelea mji huo ni kutekeleza hilo. Nitajaribu kuongea na wakazi kuhusu linalohitajika kufanywa na kupanga mikakati ya kuwaleta watu pamoja."

Timu ya kampeni ya Biden imesema kuwa itafanya mikutano na wakazi kwenye mji huo wa Kenosha ulioko kati magharibi mwa marekani na uliokumbwa ghasia siku chache zilizopita baada ya mmarekani mweusi, Jacob Blake kupigwa risasi mara 7 na polisi wa kizungu hapo Agosti 23.

Trump anamlaumu Biden akidai anahimiza ghasia kama hizo, suala ambalo limesababisha kukanusha vikali Jumatatu alipoutembelea mji wa Pittsburgh ikiwa ziara yake ya kwanza ya kampeni tangu kuzuka kwa janga la corona mwezi Marchi.

Jimbo la Wisconsin ni mojawapo ya majimbo muhimu kwenye uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Novemba 3.

Kwenye uchaguzi uliopita wa 2016, Trump alipata ushindi bila kutarajiwa kwenye jimbo hilo ambalo alitembelea Jumanne kinyume na matakwa ya Gavana na Meya ambao ni Wademokrat ,waliodai kuwa ziara yake ingeongeza ghasia.

Wakati akitoa hotuba yake Jumatano, Biden alimkosoa Trump kwa kusema kuwa utawala wake haujaleta chochote kwa Wamarekani akiongeza kusema kuwa yeye na waziri wake wa elimu Betsy De Vos hawajachukua hatua zozote kuelekea kufunguliwa tena kwa mashule.

Joe Biden akizungumza katika kampeni yake huko Mill 19 mji wa Pittsburgh, Pennsylvania., Jumatatu, Agosti. 31, 2020. (AP Photo/Carolyn Kaster)
Joe Biden akizungumza katika kampeni yake huko Mill 19 mji wa Pittsburgh, Pennsylvania., Jumatatu, Agosti. 31, 2020. (AP Photo/Carolyn Kaster)

Biden/ anaeleza : "Huenda Trump asichukulie swala la kurudi shule kama la dharura, lakini naamini kuwa linaathiri mamilioni ya watoto pamoja na wazazi wao. Nafikiri ni muhimu kuwalinda wanafunzi wetu, walimu , jamii zetu na kwa hivyo hii ni dharura ya kitaifa.

Sekta ya elimu hapa Marekani inahangaika juu ya namna ya kuanza mwaka wa elimu katika hali ya janga hili wakati utawala wa Trump ukihimiza shule zifunguliwe tena.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG