Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:03

Jaji Ginsburg wa mahakama kuu Marekani afariki


Jaji wa mahakama kuu ya Marekani Ruth Bader Ginsburg akizungumza mjini Washington, Feb. 10, 2020.
Jaji wa mahakama kuu ya Marekani Ruth Bader Ginsburg akizungumza mjini Washington, Feb. 10, 2020.

Ginsburg amekuwa jaji katika mahakama kuu ya Marekani tangu mwaka 1993 baada ya kuteuliwa na rais wa wakati huo Bill Clinton.

Jaji Ruth Bader Ginsburg wa mahakama kuu ya Marekani amefariki duniani Ijumaa mjini Washington. Alikuwa na umri wa miaka 87.

Ginsburg alikuwa mwanamke wa pili kuteuliwa kushika nafasi katika mahakama hiyo na hadi kufa kwake alikuwa mmoja wa majaji watatu wanawake katika mahakama hiyo ya juu kabisa nchini Marekani. Wengine ni Sonia Sotomayor and Elena Kegan.

Ginsburg alikuwa pia mmoja wa majaji wenye msimamo wa kiliberali katika mahakama hiyo yenye jumla ya majaji tisa.

Afya ya Ginsburg ilikuwa dhoofu katika miaka ya hivi karibuni, akiingia na kutoka hoispitali mara kadha. Ripoti za awali zinasema amefariki kutokana na saratani.

Trump atoa salamu za rambi rambi

Rais Donald Trump ambaye alipata habari za kifo cha Ginsburg akiwa katika mkutano wa kampeni Ijumaa alitoa taarifa ya rambi rambi muda mfupi baadaye akisema "Leo, taifa letu linaomboleza kuondokewa na "chuma" katika nyanja ya sheria." Trump aliendelea kusema maoni ya Ginsburg katika sheria hasa kuhusu usawa imekuwa chachu kwa vizazi vingi katika sheria.

Rais Trump hakusema katika taarifa yake ya Ijumaa kama ana nia ya kuteua jaji mwingine kabla ya uchaguzi mkuu wa Novemba 3 ama la.

Mara baada ya habari za kifo cha Jaji Ginsburg kuenea mamia ya waombolezaji walianza kukusanyika mbele ya mahakama ya juu mjini Washington kuomboleza kifo chake.

Ginsburg atakumbukwa kwa jinsi alivyopigania, miongoni mwa maswala mengine, haki za kijinsia ikiwa ni pamoja na malipo sawa katika ajira kwa wanaume na wanawake nchini Marekani.

XS
SM
MD
LG