Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 16:19

Maafisa usalama Uganda wasema tishio la mashambulizi bado lipo


Uganda yatahadharisha tishio la mashambulizi mengine
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:33 0:00

Uganda yatahadharisha tishio la mashambulizi mengine

Maafisa wa usalama nchini Uganda wanasema taifa hilo la Afrika bado linakabiliwa na vitisho vya mashambulizi mengine ya mabomu.

Kauli hiyo imetolewa siku moja baada ya kundi la kigaidi la Islamic State kudai kuhusika na milipuko miwili ya mabomu katika mji mkuu Kampala, yaliyouua raia wawili, ofisa mmoja wa polisi na kujeruhi watu wengine 33, huku baadhi yao wakiwa mahtuti.

Kundi la IS limesema lilihusika na mashambulizi hayo mjini Kampala. Wakitumia mtandao wa kijamii kutuma ujumbe wa telegram.”

IS imedai kulikuwa na zaidi ya vifo 30 na majeruhi kutokana na milipuko ya mabomu hayo.

Lakini kwa mujibu wa taarifa rasmi zilizotolewa Uganda, milipuko hiyo ya Jumanne imeuua raia watatu pamoja na washambuliaji watatu wa kujitoa muhanga, na zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa.

Mtu wanne tayari amekamatwa akituhumiwa kuhusika na mashambulizi hayo. Hii ni mara ya tatu IS kudai kuhusika na mashambulizi nchini Uganda tangu mwezi Octoba mwaka 2021.

Rais Yoweri Museveni kwenye ukurasa wa Twitter jana amelaani mashambulizi hayo na kusema kuwa yanafanywa na “ wajukuu waliochanganyikiwa”.

XS
SM
MD
LG