Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 07:05

Maelfu waandamana Addis Ababa kumuunga mkono Abiy Ahmed


Maelfu ya watu walijumuika mjini Addis Ababa, Jumapili kumuunga mkono Waziri mkuu Abiy Ahmed na serekali yake wakati vikosi vya serekali kuu vikipambana na vikosi vinavyotishia kusonga mbele mpaka mji mkuu.

Baadhi ya watu walioandamana waliipinga Marekani, moja ya mataifa ya nje ambayo yametaka kusimamishwa mapigano ya vita virefu vya mwaka mmoja.

Vita hivyo vimeongezeka baada ya vikosi vya Tigray na Oromo kudai kusonga mbele katika wiki iliyopita.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa, Umoja wa Afrika, Kenya, na Uganda pia zimetaka kusimamishwa kwa mapigano ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu.

Canada ambayo imeita hali ya Ethiopia kuwa inayobadilika kwa haraka na kuwa mbaya imeondoa familia za wafanyakazi wake wa ubalozi na wafanyakazi wasio wa lazima wamerudishwa nyumbani kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya taifa hilo ya Jumapili.

XS
SM
MD
LG