Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 02:34

Kenya yaimarisha ulinzi kufuatia shambulizi la kigaidi Uganda


Jiji la Nairobi, Kenya.
Jiji la Nairobi, Kenya.

Serikali ya Kenya imesema usalama umeimarishwa kote nchini humo kufuatia shambulizi la kigaidi katika nchi Jirani ya Uganda.

Msemaji wa serikali ya Kenya Cyrus Oguna amewasihi Wakenya kuwa waangalifu na kuripoti kisa chochote kinachozua mashaka.

Tahadhari ya Kenya inatolewa siku tatu baada ya wafungwa watatu waliopatikana na makosa ya ugaidi kutoroka kutoka katika gereza lenye ulinzi mkali la Kamiti, karibu na jiji la Nairobi.

Shambulizi la mabomu ya kujitoa mhanga yaliua watu watatu katika jiji la Kampala, Uganda Jumanne asubuhi.

Kundi la kigaidi la Islamic State limedai kuhusika na shambulizi hilo.

XS
SM
MD
LG