Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 10, 2024 Local time: 12:34

Korea Kusini : Kesi ya Rais wa zamani Park yaibuka tena


Rais wa zamani Park Geun-hye alipofikishwa mahakamani huko Seoul, Korea Kusini, Agosti 25, 2017.
Rais wa zamani Park Geun-hye alipofikishwa mahakamani huko Seoul, Korea Kusini, Agosti 25, 2017.

Mahakama ya Juu ya Korea Kusini imeamrisha mahakama ya chini ifikirie tena moja ya mashtaka ya jinai dhidi ya Rais wa zamani Park Geun-hye ambaye alilazimishwa kuondoka madarakani mwaka 2017 kutokana na kashfa ya ufisadi.

Park mwenye umri wa miaka 67 alihukumiwa mwaka 2018 kwa kutumia madaraka vibaya, kutumia mabavu na rushwa na kuhukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 24, ambapo mahakama ya rufaa iliongoeza kifungo hicho kwa mwaka mmoja.

Lakini mahakama kuu ilitoa uamuzi Alhamisi kwamba rais wa zamani huyo ahukumiwe tena kwa mashtaka ya rushwa pembeni ya mashtaka mengine aliyohukumiwa kwayo.

Park alikuwa ametuhumiwa kwa kushirikiana na rafiki yake wa karibu, Choi Soon-sil, kwa kuyalazimisha makampuni makubwa ya kimataifa, kama vile Samsung, kuchangia mabilioni ya dola za Marekani kwa mashirika mawili yasiyo ya kibiashara yaliyokuwa chini ya himaya ya Choi.

Mahakama ya Juu hiyo pia imetoa amri kwa mahakama ya rufaa irejee mara nyengine uamuzi wake wa kumpa mrithi wa Samsung Lee Jae-yong miaka miwili na nusu ya kuahirishwa kwa hukumu katika kesi hiyo.

Lee, makamu mwenyekiti wa Samsung Electronics, alihukumiwa mwaka 2017 kutokana na makosa ya rushwa na ubadhirifu na awali alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitano.

Waendesha mashtaka walimtuhumu Lee kwa kumhonga Choi ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kumrithi baba yake katika kuongoza kampuni hiyo.

Choi Soon-sil alihukumiwa mwaka 2018 kwa kosa la rushwa na hivi sasa anatumikia kifungo cha miaka 20. Mahakama ya Juu pia inapeleka hukumu yake ya awali ili ipitiwe tena na mahakama ya chini.

Hukumu iliyotolewa kwa Park ilifanya kashfa yake kuwa ya juu kuliko zote ambayo ilipelekea kiongozi huyo aliyechaguliwa kidemokrasia wa Korea Kusini kulazimika kuachia madaraka mwaka 2017, wakati Mahakama ya Katiba ya taifa hilo ilikubali kuwa Bunge la Taifa kupiga kura ya kumuondoa madarakani katika miezi ya awali.

XS
SM
MD
LG