Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 12:14

Mrithi wa kampuni ya Samsung akana makosa


Lee Jae-yong

Mrithi wa kampuni kubwa ya kimataifa ya Samsung ametangaza kuwa hana makosa baada ya kukabiliwa na tuhuma zinazofungamana na kashfa ya kisiasa inayoweza kupelekea Rais Park Geun-hye kuondolewa madarakani huko Korea Kusini.

Mwanasheria wa Lee Jae-yong aliwasilisha hati ya kisheria ya utetezi kwa niaba ya mteja wake Alhamisi.

Makamu mwenyekiti huyo wa Samsung Electronics wa Korea Kusini, mwenye umri wa miaka 48 ambae bado anashikiliwa na vyombo vya dola baada ya kukamatwa mwezi uliopita anatuhumiwa kwa makosa ya rushwa, ubadhirifu, ufisadi na kudanganya.

Waendesha mashtaka wanadai kwamba Lee alitoa milioni za dola kwa taasisi mbili zisizo za kibiashara zinazotiliwa mashaka, ambazo zinaendeshwa na Choi Soon-sil rafiki wa karibu wa Park, kwa kuitaka serikali ifanye uamuzi utao irahisishia kampuni ya Samsung kuunganisha washirika wake wawili, bila ya kujali uwezekano wa kusababisha hasara ya dola milioni 100.

Kwa kuwaunganisha washirika hao wawili ingemrahisishia Lee njia ya kuweza kumiliki Kampuni hiyo kubwa ya Samsung kutoka kwa baba yake ambaye ni mgonjwa.

Park inawezekana akawa ndio rais wa kwanza wa Korea Kusini aliyechaguliwa kidemokrasia kuondolewa madarakani iwapo Mahakama ya katiba itaendeleza uamuzi wake kwamba aondolewe madarakani kama ilivyopitishwa December.

XS
SM
MD
LG