Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:29

Mmiliki wa Samsung Ashtakiwa Kwa Kosa la Ufisadi


Milionea ambaye ni mrithi wa shirika kubwa la Samsung la Korea ya Kusini amefunguliwa mashtaka kwa tuhuma za rushwa.

Hali kadhalika mfanyabiashara huyu anakabiliwa na tuhuma za ubadhirifu ufisadi, na kashfa ambayo pia imehatarisha mustakbali wa serikali ya Rais Park Geun-hye.

Kiongozi wa Samsung, Lee Jae-yong, alifunguliwa mashtaka Jumanne pamoja na watendaji wanne wa kampuni hiyo.

Waendesha mashtaka walitumia miezi kuiandaa kesi dhidi ya Lee, wakidai kuwa alihusika katika malipo ya dola milioni 37 yaliofanywa na watendaji wa Samsung kwa rafiki wa kiongozi wa Korea, ikiwa ni njama za kupata msaada wa serikali katika kuwaunganisha washirika wawili ikiwa ni hatua ya kuimarisha udhibiti wa kampuni zote za Samsung Electronics.

Lee mwenye umri wa miaka 48, ambaye anakabiliwa na kifungo cha miaka mingi, amekana kufanya kosa lolote, kama alivyo kataa Park na Msiri wake, Choi Soon-sil.

Mchambuzi wa Korea Kusini anasema kuwa Lee, hata kama akifungwa, kunauwezekano mkubwa wa kuendelea kuiendesha kampuni hiyo akiwa jela kama walivyofanya huko nyuma watendaji wengine wa makampuni waliokuwa wamefungwa.

Lee alikamatwa katikati ya mwezi Februari, na waendesha mashtaka hawakunang’aniza kufunguliwa mashtaka dhidi yake mpaka ilipofika tarehe ya mwisho waliopewa kufanya hivyo siku ya Jumanne.

Alichukua madaraka ya Samsung kutoka kwa baba yake mgonjwa mwaka 2014, akiangalia vitega uchumi vyake vyote ambavyo vinaunganisha bustani za burudani, bima ya maisha na makampuni ya dawa.

Timu maalumu ya waendesha mashtaka iliopewa kazi ya kuchunguza kesi hii pia ilimshutumu Lee kwa kuficha vitega uchumi vilivyoko nje ya nchi na kudanganya mbele ya bunge.

Park alifunguliwa mashtaka baada ya kujulikana kashfa hiyo, iliyosimamiwa na Mahakama ya Katiba ambayo inatarajiwa kutoa uamuzi katika wiki chache iwapo aondolewe madarakani.

Atakuwa ni kiongozi wa kwanza aliyechaguliwa katika mfumo wa demokrasia kuondolewa madarakani.

President Park alishtakiwa na kusimamishwa kazi Disemba kwa tuhuma kwamba alishirikiana na rafiki yake Choi akiyarubuni makampuni makubwa ya nchi hiyo kuchangia hadi dola milioni 70 kwa taasisi mbili zinazoshukiwa uhalali wake zinaoendeshwa na Choi.

XS
SM
MD
LG