Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 07:03

Park aomba msamaha, aahidi kutoa ushirikiano katika uchunguzi


Park Geun-hye, kulia, akiwasili kwenye ofisi ya mwendesha mashtaka
Park Geun-hye, kulia, akiwasili kwenye ofisi ya mwendesha mashtaka

Rais wa Korea Kusini aliyeondoshwa madarakani Park Geun-hye amehojiwa Jumanne kufuatia kashfa ya rushwa iliomlazimisha kuachia madaraka.

“Naomba radhi kwa watu wote,” amesema wakati alipokuwa anawasili katika ofisi ya mwendesha mashtaka. “Niko tayari kwa moyo mkunjufu kushirikiana katika uchunguzi.”

Mahakama ya Katiba ya Korea Kusini ilimuondoa Park madarakani mapema mwezi huu baada ya wabunge kutuhumu kutokana na madai kuwa alishirikiana na rafiki yake wa muda mrefu Choi Soon-sil kuyarubuni makampuni kuchangia dola za Kimarekani milioni 70 kutoka taasisi zenye kutiliwa mashaka kwa matarajio ya kuwafanyia lile watalokuwa wanataka.

Park anaweza kukabiliwa na kosa la vitisho, rushwa na makosa mengine ya jinai. Lakini amekanusha kutenda kosa lolote.

Watu wengine maarufu tayari wamekwisha funguliwa mashtaka kutokana na kesi hiyo, akiwemo Lee Jae-yong, mrithi wa Kampuni kubwa ya Samsung.

Kwa kuondolewa Park madarakani, Korea Kusini itamchagua rais mpya. Serikali imetangaza kuwa uchaguzi utafanyika mei 9.

Mahakama ya Katiba nchini Korea Kusini ilipiga kura kwa kauli moja kukubaliana na uamuzi wa kumuondoa madarakani Rais Park Guen-hye.

Kaimu Jaji Mkuu Lee Jung-mi alitoa uamuzi wa mahakama ya Katiba huko Seoul, mpema mwezi huu ambayo yalitangazwa mubashara na vyombo vya habari vya taifa hilo.

“Tunaamini kuwa kunafaida nyingi kwa kumuondoa mshtakiwa katika wadhifa wake. Kwa hiyo kwa kura ya pamoja majaji wote tumetangaza kukubaliana na uamuzi wa kwanza uliofanywa na bunge wa kumuondoa rais madarakani. Mshtakiwa Rais Park Guen-hye ameondolewa madarakani.”

XS
SM
MD
LG