Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:15

Kifo cha Amini: Maandamano, migomo Iran yaingia wiki ya tatu tangu ghasia kuanza


Siku ya Jumamosi, Oct. 1, 2022, picha hii imepigwa na mtu ambaye siyo mfanyakazi wa shirika la habari la Associated Press na kupatiwa mfanyakazi wa AP nchini Iran, vyombo vya usalama vimepiga bomu la machozi kuwatawanya waandamanaji mbele ya
Chuo Kikuu cha Tehran, Iran.
Siku ya Jumamosi, Oct. 1, 2022, picha hii imepigwa na mtu ambaye siyo mfanyakazi wa shirika la habari la Associated Press na kupatiwa mfanyakazi wa AP nchini Iran, vyombo vya usalama vimepiga bomu la machozi kuwatawanya waandamanaji mbele ya Chuo Kikuu cha Tehran, Iran.

Waandamanaji waliandamana kote  nchini Iran na migomo imeripotiwa katika mkoa wa Kikurdi nchini humo siku ya  Jumamosi wakati maandamano dhidi ya kifo cha msichana akiwa chini ya ulinzi wa polisi yakiingia wiki ya tatu.

Maandamano, yaliyochochewa na kifo cha Mahsa Amini, mwenye umri wa miaka 22 kutoka eneo la Kurdistan nchini Iran, yamesambaa na kuonyesha upinzani mkubwa sana kwa mamlaka ya uongozi wa kidini Iran tangu 2019, huku darzeni wakiuawa katika ghasia zilizoenea nchi nzima.

Watu waliandamana mjini London na Paris na kwingineko siku ya Jumamosi kuwaunga mkono waandamanaji nchini Iran, baadhi yao wakibeba picha za Amini, ambaye alikufa siku ya tatu baada ya kukamatwa na polisi wa maadili wa Jamhuri ya Kiislam kwa “kutovaa inavyotakiwa.”

Nchini Iran, picha katika mitandao ya kijamii zilionyesha mikusanyiko ya watu katika miji mikubwa ikiwemo Tehran, Isfahan, Rasht na Shiraz.

Katika wilaya ya biashara ya Bazaar, mjini Tehran, waandamanaji wanaoipinga serikali walipaza sauti wakisema “tutauawa moja baada ya mwingine kama hatutaungana,” wakati kkwingineko waliweka vizuizi katika barabara kuu wakitumia wavu uliochanwa kutoka katika hifadhi ya katikati ya mji, video zilizosambazwa na akaunti ya Twitter ya Tavsir1500 iliyokuwa na wafuasi wengi zilionyesha.

Wanafunzi pia waliandamana katika vyuo vikuu mbalimbali. Katika Chuo Kikuu cha Tehran, darzeni walikamatwa, Tavsir1500 ilisema. Shirika rasmi la habari la Fars lilisema baadhi ya waandamanaji walikamatwa katika uwanja karibu na chuo kikuu.

Tavsir1500 pia imebandika kile ilichosema ni video iliyopigwa katika milango ya Chuo Kikuu cha Isfahan huku milio ya risasi ilikuwa inasikika. Picha nyingine ya video ilionyesha gesi ya kutoa machozi ikifyatuliwa kuelekea chuo kikuu hicho, kulitawanya kundi la watu.

Shirika la Habari la Reuters halikuweza kuthibitisha ripoti hizo za mitandao ya kijamii.

Maandamano hayo yalianza siku ya maziko ya Amini Septemba 17 na kuenea katika majimbo 31 ya Iran, ikiwa na tabaka zote za jamii, ikiwemo makabila na dini za waliowachache, wakishiriki na wengi wao wakidai kuangushwa kwa Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei.

Shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International, limesema kamatakamata inayofanywa na serikali dhidi ya waandamanaji imepelekea hadi hivi sasa vifo vya watu takriban 52, huku mamia wakiwa wemajeruhiwa. Makundi ya haki za binadamu wanasema darzeni ya wanaharakati, wanafunzi na wasanii wamekamatwa.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG