Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 21:35

Rais wa Ufaransa afanya mazungumzo na mwenzake wa Iran


Rais wa Iran Ebrahim Raisi akihudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran. Agosti 29, 2022.WANA.
Rais wa Iran Ebrahim Raisi akihudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran. Agosti 29, 2022.WANA.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alifanya mazungumzo ya ana kwa ana na mwenzake wa Iran Rais Ebrahim Raisi Jumanne huku kiongozi huyo wa Ufaransa akisema anatumai kuwa na uwezo wa kujadili masuala yote muhimu.

Mkutano huo ni wa kwanza kwa Raisi kukutana ana kwa ana na kiongozi mkuu wa nchi za Magharibi tangu achaguliwe mwaka jana.

Unafanyika wakati mazungumzo ya kufufua mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 yamekwama na wakati maandamano yanaongezeka nchini Iran kutokana na kifo cha Mahsa Amini, mwenye umri wa miaka 22, ambaye aliingia katika koma na kufariki dunia baada ya kukamatwa huko Tehran wiki iliyopita na polisi wa maadili kwa mavazi yasiyofaa.

Ufaransa ilisema Jumatatu kwamba hakutakuwa na pendekezo bora zaidi kwa Iran kufufua makubaliano ya nyuklia na mataifa yenye nguvu duniani na ni juu ya Tehran kufanya uamuzi sasa. Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell, ambaye anaratibu mazungumzo hayo, alisema anaona uwezekano mdogo wa maendeleo katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

XS
SM
MD
LG