Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 09:03

Maafisa wa usalama Iran wawakamata waandishi, waandamanaji wengi wao wanawake


Maombi yafanyika California kumkumbuka Mahsa Amini aliyekufa akiwa ameshikiliwa katika kituo cha polisi nchini Iran.

Wakati maandamano nchini Iran kufuatia kifo cha mwanamke kijana aliyekuwa chini ya ulinzi wa polisi yakisambaa takriban katika miji 80, mamlaka zimejibu kwa  kuwakamata waandamanaji na waandishi wa habari, wengi wao wanawake.

Mpaka kufikia siku ya Ijumaa, vikundi vya kutetea haki za vyombo vya habari vinavyofuatilia kukamatwa kwa waandishi ambao walikuwa wanaripoti kifo cha Mahsa Amini, 22, na maandamano yanayoendelea wamerekodi kukamatwa kwa waandishi takriban 28.

Watu wakishiriki katika maandamano dhidi ya utawala wa Kiislam Iran mjini New York, Marekani, Septemba 27, 2022, kulaani kifo cha Mahsa Amini akiwa kituo cha polisi nchini Iran.
Watu wakishiriki katika maandamano dhidi ya utawala wa Kiislam Iran mjini New York, Marekani, Septemba 27, 2022, kulaani kifo cha Mahsa Amini akiwa kituo cha polisi nchini Iran.

“Katika mgogoro unaoendelea – maandamano kufuatia kifo cha Mahsa Amini – tumeshuhudia ukandamizaji ambao haujawahi kutokea kwa vyombo vya habari, na tunawaona wanawake ndio walengwa wakuu,” Kiran Nazish alisema, mkurugenzi muasisi wa Muungano wa Wanawake Walio Katika Uandishi wa Habari (CFWIJ), taasisi ya mashinani ambayo imejikita kuwatetea waandishi wanawake na LGBTQ.

Nazish aliiambia VOA kuwa licha ya CFWIJ kuweza kuthibitisha maeneo kadhaa wanayoshikiliwa waandishi, “ hatufahamu ni mamlaka zipi zimewakamata” waandishi wengine.

Nchini Iran, alisema, “ Waandishi wanafungwa jela na baadae kutoweka.”

Kamati ya Kutetea Waandishi wa Habari (CPJ) yenye makao yake New York, ambayo pia inafuatilia ukamataji huo, ilisema kuwa wengi wao wanachukuliwa kutoka majumbani mwao wakati wa usiku na maaskari ambao hawaonyeshi nyaraka zozote za mahakama au hati ya kuwakamata. Wengi waliokamatwa hawajafunguliwa mashtaka rasmi.

XS
SM
MD
LG