Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 18:52

Je, ni sawa kupokea taarifa dhidi ya hasimu wako kisiasa Marekani?


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Mzozo unaofukuta juu ya maoni ya Rais wa Marekani Donald Trump juu ya “tafiti dhidi ya hasimu wake”- kwamba yuko tayari kupokea msaada wa kisiasa kutoka serikali ya kigeni -limeibua swali hili :

Je, tafiti dhid ya upinzani ni “kitu chenye umuhimu” na kwamba raia wa kigeni hawanaruhusa kutoa msaada kwa kampeni za kisiasa za Marekani?

Mahojiano na Kituo cha ABC

Katika mahojiano na Kituo cha televisheni cha ABC Jumatano, Trump atatafakari iwapo achukuwe taarifa iliyoandaliwa raia wa kigeni ambayo huenda ikamsaidia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa 2020 atapogombea tena.

“Hakuna kosa lolote kusikiliza taarifa hiyo,” Trump alisema. “Ikiwa mtu amekufikia kutoka nchi nyingine – Norway – ‘Tunataarifa juu ya hasimu wako wa kisiasa.’ Oh. Nafikiria nitataka kusikia taarifa hiyo.”

Tume ya Uchaguzi yatoa tamko

Lakini taharuki iliyosababishwa na maneno yake Trump ilikuwa inatosha kumsukuma Ellen Weintraub, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Serikali Kuu, kutoa tamko akisisitiza katazo lilioko la muda mrefu Marekani linalopiga marufuku mtu yeyote kupokea msaada wa kigeni katika uchaguzi wa Marekani.

“Nataka niweke wazi kwa asilimia 100 kwa umma wa Marekani na mtu yeyote anaingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa ofisi ya umma : Ni kinyume cha sheria kwa mtu yeyote kuomba, kukubali au kupokea kitu chochote cha thamani kutoka kwa raia wa kigeni kinachofungamana na uchaguzi wa Marekani,” Weintraub, ambaye aliteuliwa na Rais mstaafu George W. Bush aliandika.

Sheria ya uchaguzi

Sheria ya uchaguzi ya Marekani inapiga marufuku raia wa kigeni kutoa – na kampeni za Marekani kuomba au kupokea – “mchango wowote au msaada wa fedha au kitu chochote cha thamani.

Sheria hiyo haisemi nini kinachofanya kiwe “kitu cha thamani.” Lakini, kanuni za FEC zinatambua “kila kinachochangiwa” iwe nafasi ya ofisi, zana na huduma za matangazo “kuwa ni vitu vya thamani.”

XS
SM
MD
LG