Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 07:45

Balaa la udukuzi wa mitandao laingia siku ya pili duniani


Kompyuta iliyoathiriwa na uvamizi wa kimitandao nchini Ujerumani kwenye kituo cha treni.
Kompyuta iliyoathiriwa na uvamizi wa kimitandao nchini Ujerumani kwenye kituo cha treni.

Uvamizi wa kutisha wa udukuzi wa mifumo ya kompyuta (Cyberattack) umeathiri maelefu ya mitandao katika nchi mbalimbali duniani, kwa kuingiliwa na virusi aina ya malware ambayo inafunga mafaili ya kompyuta na kudai fidia.

Tishio hilo la udukuzi limeendelea katika siku ya pili Jumamosi, wakati juhudi za uchunguzi bado hazikuzaa matunda katika kujua nani aliyeanzisha vita hii.

Uvamizi wa kutisha wa udukuzi huo wa mifumo ya kompyuta uliotokea kwa muda kidogo na kushika kasi ya ajabu siku ya jana – umezikumba pia nchi za Afrika.

Wataalamu wa usalama wa mifumo ya kompyuta wamewahakikishia watumiaji wa kompyuta ambao walikuwa wamehakikisha kuwa wamejadidisha mifumo ya “PC operating systems” watakuwa wamenusurika kwa kiasi fulani.

Wataalamu wameshauri kuwa wale wote ambao mitandao yao ilifungwa na kirusi kinachojulikana kama ransomware wasifanye malipo yoyote waliotakiwa na wahalifu hao wa mitandao, ambazo ni Dola za Kimarekani 300.

Fedha hizo zinazotakiwa kulipwa katika sarafu za kidigitali zijulikanazo kama bitcoin, mfumo ambao unapeleka fedha hizo katika kituo cha fedha kisichojulikana chenye herufi nyingi na nambari.

Hata hivyo watayarishaji wa kirusi hicho cha kidukuzi cha “WannaCry” ransomware chenye kufanya mashambulizi wamewaambia waathirika wake kiwango cha fedha kitaongezeka iwapo hawatofuata maelekezo katika siku tatu tangu udukuzi huo utokee- ikiwa ni Jumatatu kwa wengi walioathiriwa.

Aidha wadukuzi hao wameonya kuwa iwapo watu hawatotii amri yao watafuta mafaili yote katika mfumo wa kompyuta hizo zilizoathirika iwapo malipo hayatofanyika katika kipindi cha siku saba.

Avast, ambayo ni kampuni inayotengeneza 'software' za ulinzi imedai kuwa inawatumiaji milioni 400 duniani, na imesema imebaini kirusi hicho cha ransomware kilichoshambulia, kiliongezeka kwa kasi siku ya Jumamosi kufikia dukuzi 57,000.

Avast ambayo iliasisiwa mwaka 1988 na watafiti wa Czech, imesema idadi kubwa ya udukuzi huo uliilenga Russia, Ukraine na Taiwan, lakini taasisi kubwa katika nchi nyingi duniani ziliathirika pia.

XS
SM
MD
LG