Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 19:33

Japan yawaenzi wahanga wa bomu la atomic


Bomu la Atomic
Bomu la Atomic

Majira ya saa tano asubuhi huko Nagasaki, manusura wa tukio hilo na wengine walisimama kimya kwa dakika moja kuwaenzi zaidi ya watu 70,000 waliokufa wakati ndege ya kivita B-29 Bockscar ilipoangusha bomu la aina ya kemikali ya plutonium lenye tani 4.5, ambalo lilipewa jina la “Fat Man” katika mji huo.

“Kama nchi ambayo imepitia kihoro cha silaha za nyuklia, tafadhali wekeni saini katika mkataba unaopiga marufuku silaha za nyuklia na hakikisheni inapata maridhiano mapema iwezekanavyo,” amesema meya wa Nagasaki Tomihisa Taue.

Pia tafadhali upitieni mpango wa kuweka kanda zitakazo kuwa hazina silaha za nyuklia katika eneo la Kaskazini mashariki ya bara la Asia.

Tafadhalini mdumu katika kushikamana na misingi ya amani ya katiba ya Japan, ikiwemo azma ya kutoanzisha vita.”

Waziri Mkuu Shinzo Abe aliweka shada la maua katika eneo hilo la kumbukumbu kuwaenzi wahanga hao na kutoa hotuba lakini aliepuka kuutaja mkataba huo moja kwa moja.

“Maafa yaliyoipata Nagasaki na Hiroshima na madhila yaliosababishwa na bomu hilo kwa watu wake lazima yasijirudie tena,” Abe alisema.

“Ikiwa ni nchi pekee iliyoathiriwa na silaha za nyuklia wakati wa vita, ujumbe huu utaendelea kutobadilika katika taifa letu ili tuweze kusonga mbele hatua kwa hatua juhudi za jumuiya ya kimataifa kufikia hali ya kutokuwepo silaha za nyuklia duniani.

Japan haijasaini mkataba huo. Manusura wengi walianza kuugua saratani na magonjwa mengine kwa sababu ya athari za mionzi ya nyuklia.

Makamu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa ngazi ya juu wa masuala ya kusitisha silaha za maangamizi Izumi Nakamitsu amesema katika ujumbe wake katika kumbukumbu ya Nagasaki Peace Memorial kwamba dunia “ni lazima irejee katika uelewa ya kuwa katika vita vya nyuklia hakuna anayeshinda na lazima visitokee,” akiongeza “kuna ulazima kuzuia kufutika kwa utaratibu huo wa kuzuia silaha za nyuklia.

Nchi zote zilizokuwa na silaha za nyuklia zinawajibika kuongoza utekelezaji wa utaratibu huo.”

XS
SM
MD
LG