Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 04:39

Idadi ya maambukizi ya COVID-19 yakaribia milioni 1 Afrika


Majeneza ya waliokufa kutokana na COVID-19 yakisubiri kusafirishwa kwa ajili ya mazishi Afrika Kusini wakati nchi hiyo ikiwa katika amri ya kutotoka nje kutokana na janga la corona, huko Soweto, Kusini magharibi ya Johannesburg, Afrika Kusini Agosti 4, 2020.REUTERS/Siphiwe Sibeko
Majeneza ya waliokufa kutokana na COVID-19 yakisubiri kusafirishwa kwa ajili ya mazishi Afrika Kusini wakati nchi hiyo ikiwa katika amri ya kutotoka nje kutokana na janga la corona, huko Soweto, Kusini magharibi ya Johannesburg, Afrika Kusini Agosti 4, 2020.REUTERS/Siphiwe Sibeko

Idadi ya watu wanaoambukizwa ugonjwa wa COVID-19 barani Afrika inakaribia milioni moja wiki hii, huku Afrika Kusini ikwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya wagonjwa wanaofikia nusu milioni.

Maafisa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wanasema wanapeleka timu ya wataalamu huko Afrika hivi karibuni wakati waziri wa afya akionya kwamba nchi yake inaweza kushuhudia wimbi la pili la Maambukizi.

Miezi mitano baada ya mtu wa kwanza kupimwa na kupatikana na virusi vya corona huko Afrika, bara hilo lingali na idadi ndogo zaidi ya wagonjwa ukilinganisha na mabara mengine ya dunia ikiwa na asilimia 5 tu ya wagonjwa wote milioni 4 laki 9 hii leo.

Dkt Matshiodisho Moeti mkurugezi wa kanda ya Afrika kwa ajili ya WHO anasema maafisa wa bara hilo wana wasiwasi kuhusiana na kitovu cha sasa cha Maambukizi Afrika Kusini na bara zima kwa ujumla wakati idadi inakaribia milioni moja.

Dkt Moeti anafafanua : "Inaanza kudhihirika kwamba tutaishi na virusi hivi kwa muda mrefu. Kuna karibu wagonjwa milioni moja waloripotiwa Afrika, na zaidi ya elfu 21 kwa usikitifu wamefariki. Afrika kusini inaendelea kua nchi inaoathirika zaidi barani humo ikiwa ni ya tano duniani kote. Kwa ushirikaina na wizara yake ya afya tunawapeleka waatalam 40 kuisaidia nchi hiyo."

Pia amesema waatalamu wa afya wana wasiwasi kutokana na uwezekano wa idadi kuwa kubwa zaidi kuliko ilivyo hivi sasa kwa sababu ya ukosefu wa vifaa vya kupima na vizingiti vingine.

Mkurugenzi wa WHO wa Kanda ya Afrika anaongeza kuwa : "Mmoja kati ya changamoto kubwa inayotiya wasi wasi katika nchi nyingi za afrika ni upungufu wa vyombo vya kupima watu kwa ajili ya Covid 19. Wakati huo huo kuna baadhi ya nchi zilizoimarisha uwezo wao wa kupima na hivyo kupunguza maambukizi kama vile Mauritius, Rwanda, cape Verde na Botswana.

Waziri wa afya wa Afrika kusini Dk Zweli Mkhize anasema masharti makali ya kusitisha shughuli zote mnamo wiki 9 zimesaidia kupunguza kasi ya maambukizo lakini anasema Ikiwa nchi hiyo haitaendelea na juhudi zake basi wimbi la pili liko karibu.

Nchini Rwanda waziri wa afya anasema maafisa wanatafuta njia mpya za kutibu wagonjwa na kuwa na mpango wa kuwa tayari kitaifa ambao hadi sasa umegharimu dola milioni 73.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG