Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 02:42

Mawaziri 3 waambukizwa COVID-19 Gambia


Ramani ya nchi ya Gambia
Ramani ya nchi ya Gambia

Mawaziri watatu nchini Gambia wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona.

Habari kutoka ofisi ya rais Adama Barrow imethibitisha habari hizo, dhihirisho la kwamba virusi hivyo vinaendelea kusambaa kwa kasi nchini humo, makamu wa rais akiwa amewekwa karantini baada ya kugunduliwa kuambukizwa wiki iliyopita.

Rais Adama Barrow yupo karantini ya wiki mbili baada ya makamu wake Isatou Touray kugunduliwa kuambukizwa virusi vya Corona.

Mawaziri ambao wameripotiwa kuambukizwa ni waziri wa fedha Mambureh Njie, waziri wa nshati Fafa Sanyang na waziri wa kilimo Amie Fabureh.

Hakuna taarifa zaidi imetolewa kuhusu hali ya afya ya mawaziri hao.

Gambia, nchi ndogo sana Afrika, imeripoti kuna watu 498 waloambukizwa na virusi vya Corona hadi tunapo tayarisha ripoti hii.

Vifo 19 vimeripotiwa katika nchi hiyo ya Afrika magharibi.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Kennes Bwire, Washington DC.

XS
SM
MD
LG