Jeshi la Iran la anga lina darzeni chache za ndege za kivita, ikiwemo ndege za kivita za Russia na zile kongwe za Kimarekani zilizo nunuliwa kabla ya Mapinduzi ya Kiislam ya mwaka 1979.
“Mipango imekamilika ya kupokea ndege za kivita aina ya Sukhoi Su-35, helikopta za mashambulizi aina ya Mil Mi-28, na ndege za mafunzo za kivita aina ya Yak-130 ambazo zitakuwa sehemu ya vikosi vya mashambulizi vya Jeshi la Iran,” naibu waziri wa ulinzi wa Iran Mehdi Farahi alisema.
Ripoti iliyotolewa na Tasnim haikujumuisha uthibitisho wowote kutoka Russia kuhusu makubaliano hayo.
Mwaka 2018, Iran ilisema imeanza kutengeneza aina ya ndege ya kivita iliyobuniwa nchini kwa ajili ya matumizi katika jeshi lake la anga.
Wataalam wa kijeshi wanaamini ndege hiyo ya kivita ni igizo la ndege aina ya F-5, ambayo ilitengenezwa hapo awali nchini Marekani katika miaka ya 1960.
Habari hii imetokana na shirika la habari la Reuters
Forum