Shambulio la Ijumaa kwa CMA CGM linakuja wakati usafiri wa meli za kimataifa unazidi kujikuta ukilengwa katika vita vya wiki nzima ambavyo vinatishia kuwa mzozo mpana wa kikanda hata wakati makubaliano ya amani yamesimamisha mapigano na Hamas ili kubadilishana mateka na wafungwa wa Kipalestina walioko Israeli.
Afisa huyo wa ulinzi, ambaye alizungumza na The Associated Press kwa sharti la kutotajwa jina kuzungumzia masuala ya kijasusi, alisema meli hiyo iliyokuwa na bendera ya Malta ilishukiwa kulengwa na ndege isiyo na rubani ya Shahed-136 yenye umbo la pembetatu, iliyokuwa na bomu ikiwa katika maji ya kimataifa. Ndege hiyo isiyo na rubani ililipuka na kusababisha uharibifu kwenye meli hiyo lakini haikujeruhi mabaharia wake.
Forum