Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 13, 2025 Local time: 13:22

Moto umezuka Iran na kuuwa watu 32 na kuwajeruhi 16


Mfano wa kituo kilichoshika moto nchini Iran cha ukarabati kwa wale wanaotumia dawa za kulevya. Aug. 13, 2023,
Mfano wa kituo kilichoshika moto nchini Iran cha ukarabati kwa wale wanaotumia dawa za kulevya. Aug. 13, 2023,

Uchunguzi wa awali umeonyesha kwamba kifaa cha kutoa joto (Heater) katika kituo hicho cha Langarud kilichopo Caspian Sea kwenye jimbo la Gilan ndiyo chanzo cha moto uliosambaa kwenye  eneo lote la kituo hicho, naibu gavana wa jimbo hilo alikaririwa akisema katika shirika la habari la Fars

Moto mkubwa umezuka katika kituo cha ukarabati kwa wale wanaotumia dawa za kulevya kaskazini mwa Iran. Umeuwa takribani watu 32 na kujeruhi 16, vyombo vya habari vya Iran vimeripoti Ijumaa.

Uchunguzi wa awali umeonyesha kwamba kifaa cha kutoa joto (Heater) katika kituo hicho cha Langarud kilichopo Caspian Sea kwenye jimbo la Gilan ndiyo chanzo cha moto uliosambaa kwenye eneo lote la kituo hicho, naibu gavana wa jimbo hilo alikaririwa akisema katika shirika la habari la Fars.

“Meneja na washukiwa wengine wamekamatwa ili chanzo cha tukio hilo kijulikana kwa usahihi zaidi” tovuti ya habari ya Tasnim ilisema.

Kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayohusika na Dawa za Kulevya na Uhalifu ni kwamba Iran ni mojawapo ya nchi zenye matatizo makubwa sana ya uraibu duniani.

Ipo kwenye njia kuu ya usafirishaji haramu wa afyuni, chanzo cha opium na herion kutoka Afghanistan kwenda Ulaya Magharibi.

Forum

XS
SM
MD
LG