Kituo hicho pia kinalaumiwa kuunga mkono juhudi za Hezbollah, serikali imesema. Wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani imesema kwamba Islamic Center Hamburg, au IZH imekuwa kwa muda mrefu chini ya uangalizi wa idara ya ujasusi wa ndani wa serikali.
Ripoti zimeongeza kusema kwamba lengo la kundi hilo ni kuendeleza juhudi za mageuzi za kiongozi wa Iran. Serikali ya Ujerumani pia inachunguza uwezekano wa kundi hilo kuunga mkono shughuli zilizopigwa marufuku nchini humo, zinazofanywa na kundi la wanamgambo la Lebanon , Hezbollah, linaloungwa mkono na Iran, tangu Hamas ilipoishambulia Israel kutoka Gaza, mwezi uliopita.
Forum