Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 06:15

IMF : Tanzania yahitaji msaada wa haraka kuepuka uchumi kuporomoka


Nembo ya Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, kama inavyoonekana katika jengo łąkę mjini Washington.
Nembo ya Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, kama inavyoonekana katika jengo łąkę mjini Washington.

Tanzania inahitaji msaada wa haraka wa fedha wa takriban dola za Marekani bilioni 1.1 (asilimia 1.5 ya pato lake la taifa) katika miezi 12 ijayo ili kuepusha uwezekano wa uchumi kuporomoka. 

Tishio hilo la kuporomoka kwa uchumi wa Tanzania unatokana na janga la COVID-19 na kupanda kwa gharama za uagizaji bidhaa kutokana na ongezeko la bei ya mafuta ghafi.

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) linasema katika ripoti yake juu ya nchi hiyo No 21/213, iliyotolewa mwezi huu wa Septemba, imesema kuwa nchi hiyo inahitaji msaada wa haraka kuimarisha ankara ya uagizaji bidhaa kutoka nje na ile ya uuzaji bidhaa nje (BOP), wakati serikali ikitekeleza mpango kabambe wa kukabiliana athari za COVID-19 kufuatia kuanguka kwa mapato ya mauzo ya nje na gharama za kuagiza bidhaa.

“Uagizaji wa dharura wa dawa, vifaa vya kupimia na vile vya kujikinga vinahitajika haraka ili kujibu wimbi la tatu la janga la corona. Kununua na kusambaza chanjo ni kipaumbele cha juu ambacho pia kinahitaji kuongeza miundombinu ya usambazaji wa chanjo,” imesema ripoti iliyoandaliwa na wafanyakazi wa IMF.

Mahitaji ya ufadhili wa ziada yamekuja baada ya Bodi ya IMF hapo Septemba 7, 2021, ilipoidhinisha kutolewa kwa dola milioni 567.25 kwa Tanzania kuisaidia nchi hiyo kugharimia kuimarisha ankara ya ununuzi na uagizaji bidhaa kutoka nje (BOP) iliyoathiriwa na COVID-19.

Akiba ya fedha za kigeni imeshuka kwa zaidi ya dola milioni 400 kufikia dola bilioni 5.2 mwezi Juni kutoka dola bilioni 5.6 mwaka 2019 wakati mapato ya utalii yakitarajiwa kubakia katika kiwango kile kilichokuwa kabla ya mgogoro.

Kadhalika makadirio ya kuongezeka kwa bei ya mafuta na bidhaa nyingine itaongeza gharama za uagizaji bidhaa na kwa sehemu fulani itaathiri mapato ya usafirishaji dhahabu nje.

Kulingana na IMF, mlipuko wa COVID-19 umepelekea kuporomoka kwa sekta ya utalii na kukuza haja ya msaada muhimu wa ufadhili kukabiliana na athari za afya na kiuchumi zilizotokana na janga la corona.

Chanzo cha Habari Hii ni gazeti la The East African la Kenya

XS
SM
MD
LG