Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 06:50

Polisi : Hamza aliyewaua maafisa polisi na mlinzi ni gaidi


Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura, Tanzania (Kwa hisani ya Global Publishers TV, Tanzania).
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura, Tanzania (Kwa hisani ya Global Publishers TV, Tanzania).

Polisi nchini Tanzania wanasema mtu mwenye silaha aliyewaua polisi watatu na mlinzi mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi katika shambulizi la bunduki Agosti 25 alikwa ni gaidi wa kujitoa muhanga. Mwandishi Charles Kombe ameripoti kutoka Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura alimtaja mtu huyo mwenye silaha kuwa Hamza Mohamed, mkazi wa Dar es Salaam mwenye umri wa miaka 33.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:10 0:00


Mohamed alipigwa risasi na kuuwawa na polisi baada ya kuua watu wanne, wakiwemo maafisa wa polisi, wiki mojo iliyopita mjini Dar es Salaam.

Wambura amesema polisi wamechunguza kile kilichomhamasisha mwenye silaha huyo na kugundua alikuwa akishiriki katika mitandao ya jamii.

Wambura amesema mshukiwa huyo alikuwa akisoma habari nyingi zilizoko katika mitandao zinazoonyesha shughuli za jumuiya za kigaidi kama vile al-Shabab na ISIS. Amesema tabia ya Mohamed imefuata mkondo wa mawasiliano yake na watu wa nchi ambazo zinajulikana kuwa na harakati za kihalifu, kama vile ugaidi. Wambura hakuzitaja nchi hizo.

Mkazi wa Dar es Salaam Eugene Michael anasema habari hizi zinaongeza wasiwasi jinsi mamlaka husika zilivyokuwa tayari kufuatilia washukiwa wa ugaidi nchini Tanzania.

Michael anasema, “Taarifa zilizotolewa hapo awali zilisema mtu huyu alikuwa mtu wa kawaida katika jamii.

Anaongeza kuwa “ripoti ya polisi inaleta hofu kwa sisi raia kwani hatuwezi kujua watu wangapi kama yeye tunaishi nao katika jamii yetu.”

Hili lilikuwa shambulizi la kwanza Tanzania ambalo mamlaka imelieleza kuwa ni la kigaidi. Nchi ilikuwa haina tukio la kigaidi, isipokuwa shambulizi la bomu la Agosti 1998 katika ubalozi wa Marekani lililofanywa na al-Qaida mjini Dar es Salaam. Bomu hilo liliuwa watu 11.

.

XS
SM
MD
LG