Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 06:03

IMF yaikopesha Tanzania dola milioni 567 kupambana na COVID-19


Nembo ya IMF ikionekana nje ya jengo hilo katika makao yake makuu mjini Washington Dc.
Nembo ya IMF ikionekana nje ya jengo hilo katika makao yake makuu mjini Washington Dc.

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) lenye makao yake  Washington DC limeidhinisha dola milioni 567 za mkopo ili kuisaidia Tanzania kupambana na COVID-19.

Shirika hilo lenye makao yake Washington DC liliidhinisha dola milioni 567 kwa msaada wa Covid kwa Tanzania, ambayo hadi hivi karibuni ilikuwa imejitenga na ulimwengu katika mapambano dhidi ya corona na ilipuuza ukubwa wa ugonjwa huo.

Uchumi wake ulipungua hadi asilimia 4.8 mwaka 2020, masharti ya kusafiri yaliiumiza sekta ya utalii, ambayo inaingiza mapato kwa kiasi kikubwa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki ambapo ukuaji ulitarajiwa kubaki vile vile mwaka 2021.

IMF ilisema Tanzania inakabiliwa na gharama za dharura za kiafya, kiuchumi na kibinadamu wakati wimbi la tatu la janga hilo lilipoikumba nchi.

Janga la Covid-19 limeathiri vibaya matarajio makuu ya kiuchumi kwa Tanzania, na afya na ustawi wa watu wake” Bo Li, naibu mkurugenzi mtendaji wa IMF, alisema katika taarifa ya kutangaza ufadhili wa dharura siku ya Jumanne.

IMF ilisema mtikisiko wa uchumi uliosababishwa na janga umeongeza umasikini na ukosefu wa ajira na kuongezeka kwa hatari ya deni, haswa kutokana na kuporomoka kwa sekta ya utalii.

Tanzania ilizindua msukumo wa utoaji chanjo ya corona mwezi Julai katika kuonyesha tofauti ya kuachana na sera za kutoamini covid za hayati rais John Magufuli, kiongozi ambaye aliudharau ugonjwa huo kwa muda mwingi wa janga.

Magufuli, ambaye mtindo wake wa uongozi ulimpatia jina la utani "Bulldozer", alizibeza chanjo zilizotengenezwa na nchi za kigeni akipendelea zaidi nguvu ya sala kwa uponyaji na kudharau barakoa na upimaji kuwa sio muhimu.

Mrithi wake Samia Suluhu Hassan, ambaye alichukua madaraka mwezi Machi baada ya kifo cha ghafla cha Magufuli, alichukua njia tofauti, kuhamasisha hatua za kuzuia kuenea kwa virusi na njia yenye mwelekeo wa kisayansi kupambana na janga hilo.

Hadi mwezi Julai, wakati Hassan alipopokea chanjo yake ya kwanza akionekana moja kwa moja, kwenye televisheni ya taifa Tanzania ilikuwa kati ya nchi tatu tu katika bara la Afrika ambazo bado hazijaanza kuwapa chanjo raia wake dhidi ya Covid 19.

XS
SM
MD
LG