Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 08:43

Dkt Stergomena L Tax mwanamke wa kwanza kuteuliwa waziri wa Ulinzi Tanzania


Mwenyekiti wa Baraza la SADC Maite Nkoana-Mashabane (L) na Katibu Stergomena Lawrence Tax (R)
Mwenyekiti wa Baraza la SADC Maite Nkoana-Mashabane (L) na Katibu Stergomena Lawrence Tax (R)

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Jumapili amemteua Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na marehemu Elias John Kuandikwa.

Dkt. Tax ni mwanamke wa kwanza nchini Tanzania kushika wadhifa katika Wizara ya Ulinzi. Hivi karibuni alimaliza muda wake akihudumu kama katibu mtendaji katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na pia amewahi kuwa katibu mkuu katika wizara mbali mbali nchini Tanzania, katika wizara za Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Viwanda, Biashara na Masoko na Fedha na Mipango.

Rais Samia pia amemteua Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ambapo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Faustine Ndugulile ambaye ameondolewa katika wadhifa huo.

January Yusuf Makamba ambaye aliwahi kushika wadhifa wa uwaziri na naibu waziri, ameteuliwa kuwa Waziri wa Nishati ambapo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Medard Matogolo Kalemani ambaye naye pia amefutwa kazi na rais.

Rais pia amemteua Prof. Makame Mnyaa Mbarawa kuwa waziri wa Ujenzi na Uchukuzi. Dkt. Leonard Madaraka Chamuhiro ambaye alikuwa akishikilia wadhifa naye amefutwa kazi.

Dkt. Aliezer Mbuki Feleshi, ameteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambapo anachukua nafasi inayoachwa wazi wa Prof. Adelardus Kilango ambaye ameteuliwa kuwa balozi. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Feleshi alikuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

XS
SM
MD
LG