Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 20:30

Idadi ya watoto wanaotumiwa kupigana vita yaongezeka Afrika Magharibi na Kati


FILE - Wanawake na watoto, walookolewa na jeshi la Nigeria baada ya kutekwa na wapiganaji wa Boko Haram wakiwa katika kambi ya Yola, Nigeria, May 3, 2015.
FILE - Wanawake na watoto, walookolewa na jeshi la Nigeria baada ya kutekwa na wapiganaji wa Boko Haram wakiwa katika kambi ya Yola, Nigeria, May 3, 2015.

Afrika Magharibi na kati zimerekodi idadi kubwa ya watoto wanaoandikishwa katika mizozo ikilinganishwa na nchi nyingine zozote duniani na idadi inaongezeka, shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa limesema.

Watoto wanatumiwa kama wapiganaji lakini pia wapeleka ujumbe, wapelelezi, wapishi, wasafishaji, walinzi na wabeba mizigo wakitumika katika makundi yenye silaha kutoka Mali hadi DRC, UNICEF imesema katika ripoti yake.

Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa watoto 21,000 wanaandikishwa na vikosi vya kijeshi na makundi mengine yenye silaha yasiyokuwa ya serikali katika eneo hilo kati ya mwaka 2016 na 2020.

Idadi ya UN iliyothibitishwa imeongezeka kwa asilimia 16 hadi 4,562 kwa watoto mwaka 2020 kutoka 3,974 mwaka 2016.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ROITA Afrika Magharibi na kati pia zina idadi kubwa ya watoto walioathiriwa na ghasia za kingono duniani na idadi kubwa ya utekaji katika kipindi hicho hicho.

Afrika Magharibi na kati inakabiliwa na migogoro mingi inayoendelea ikiwa ni pamoja na waasi wa Kiislamu wenye msimamo mkali katika eneo la Sahel na Ukanda wa Ziwa Chad.

Mzozo uko kwa wale wanaotaka kujitenga nchini Cameroon na wanamgambo wanaopigana katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

XS
SM
MD
LG