Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 04:37

Boko Haram wauwa wanajeshi 5 wa Cameroon


Wanajeshi wa Cameroon wanaokabiliana na wanamgambo kaskazini magharibi mwa nchi
Wanajeshi wa Cameroon wanaokabiliana na wanamgambo kaskazini magharibi mwa nchi

Wanamgambo wa Boko Haram wameua wanajeshi watano wa Cameroon na raia mmoja kwenye shambulizi kaskazini mwa nchi, wizara ya ulinzi ya Cameroon imesema Jumanne.

Shambulizi hilo lilifanyika Jumatatu usiku karibu na mpaka na Nigeria, ambako mashambulizi ya kundi hilo lenye itikadi kali ya kiislamu yameongezeka.

Taarifa ya wizara ya ulinzi imesema “kundi la magaidi wenye silaha nzito wa tawi la Boko Haram, wakiwa ndani ya magari kadhaa walishambulia kituo cha jeshi karibu na Kijiji cha Zigue, kilomita chache kutoka mpaka na Nigeria.

Taarifa zimeongeza kuwa baadhi ya wanamgambo waliuwawa, bila kutoa maelezo zaidi. Wapiganaji wa Boko Haram na kundi jingine lililojitenga, la Islamic State in West Africa (ISWAP), wamekua wakiendesha mashambulizi mabaya dhidi ya maafisa wa usalama na raia kaskazini mwa Cameroon, pamoja na kwenye nchi jirani za Nigeria, Niger na Chad

XS
SM
MD
LG